Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Songas wakishusha vyakula kwa ajili ya wazee wasiojiweza wa Kituo cha Nunge kilichopo Kigamboni jijini,Dar es Salaam kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya. Jumla ya Sh Milioni sita zilitumika kwa ajili ya chakula hicho kwa kaya hamsini
Wafanyakazi wa Kampuni ya Songas wakiwa wamebeba vyakula hivyo
Kaimu Mkuu wa Kituo cha makazi ya wazee wasiojiweza cha Nunge, Moses Gunza akizungumza baada ya kupokea msaada huo wa vyakula kwa ajili ya wazee hao vilivyotolewa na Kampuni ya Songas. Kushoto ni Meneja Mahusiano wa Kampuni hiyo, Nicodemas Chipakapaka.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Songas, Nicodemas Chipakapaka(kushoto) akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo wa vyakula.
Kaimu Mkuu wa Kituo cha makazi ya wazee wasiojiweza cha Nunge, Moses Gunza(kushoto) akipokea msaada wa vyakula kutoka Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Songas, Nicodemas Chipakapaka
Baadhi ya wazee wasiojiweza wa Kituo cha Nunge wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyakula vilivyotelewa na Kampuni ya Songas
Mmoja wa wazee wasiojiweza akiwa na mfuko wa vyakula alivyokabidhiwa na Kampuni ya Songas
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Songas, wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa wazee wasiojiweza wa Kituo cha Nunge.Picha Na Amani Tanzania Blog
No comments:
Post a Comment