Monday, December 24, 2012

KWELI BONGO TAMBARARE

Msanii Lady Jay Dee

SALAAM ZA KUVUNJA UKIMYA TOKA KWANGU

Ndugu, jamaa na marafiki.
Ni matumaini yangu wote mu wazima wa afya tukiwa tunaelekea kuumaliza 2012.
Nina jambo napenda kuwajulisha ambalo naona ni kheri tukishiriki sote pamoja kama watanzania.
Yeyote mwenye kuguswa na atakaeona ni vema kushiriki basi anakaribishwa. Kila siku nikiamka nyumbani iwe ni asubuhi, mchana au jioni nimekuwa nikikuta barua si chini ya 5 zote zikiwa ni za kuomba misaada mbali mbali. Kazi, Ada za shule, Chakula, muziki n.k Mbali na Barua hizo, pia nimekuwa nikipokea mails mbali mbali pia za watu wanaohitaji msaada. Nimeona kiukweli mimi siwezi kusaidia peke yangu kutokana na wingi wa barua hizo, kulinganisha na uwezo halisi nilio nao.
Wazo lililonijia ni kuweka barua na e-mail hizo hapa zisomwe na watu mbali mbali
Ili kama kuna itakaemgusa, atakae ona anaweza kusaidia moja wapo ya barua hizo basi na afanye hivyo ili kushika mikono walio chini ki uwezo.

Nitajitahidi ku post walau barua 2 -3 au email 2-3 kwa wiki. Nikipata muda, manake Diary inabana mpaka blog nishaisahau

Inawezekana wapo wasanii, yani wanaoomba lakini si kweli kuwa wana matatizo hayo. Na pia inawezekana kabisa kuwa wapo wenye shida na wanahitaji kusaidiwa.  Itakuwa ni jukumu la anaetaka kutoa msaada kufatilia na kujua ukweli halisi kutoka kwa muombaji, kwakuwa maombi mengi huambatana na namba za simu za muombaji au e-mail yake.

NAOMBA KUWASILISHA E-MAIL YA KWANZA TOKA KWA KALUNDE IBRAHIM:
From: Kalunde Ibrahim
To: Judith Wambura
Sent: Thursday, 20 December 2012, 12:03
Subject: msaada wa karo

shikamoo dada yangu,
mie ni mwanafunzi natarajia kuingia kidato cha nne mwakani, nipo mkoa wa Mara wilayani Serengeti, nasoma Nata sekondari
mie naomba msaada wa kunilipia karo ya mwakani, sihitaji unipe pesa mkononi, naomba unilipie tu mie nisome kwani nasoma kwa shida ninaishi na mama yangu naye hana uwezo wa kunilipa ada kwa muda.
pale tunalipa ada ya hostel kwa mwaka kama shs.352,000/=, ada shs.20,000/=, mlinzi shs.10,000/=
taaluma shs.10,000/=, na michango mingine midogo inakaribia shs.400,000/= kwa mwaka, kiasi hiki cha fedha kwa mama yangu ni pesa kubwa mno, nakuomba dada yangu uniwezeshe kwa hilo,

Nasubiri toka kwako,

Kalunde

Chanzo: Lady Jay Dee

2 comments:

Anonymous said...

Umefanya vizuri sana kuwasilisha hii barua kwa jamii. Nafikiri itakuwa ni changamoto kwa jamii nzima kuona jinsi gani watasaidia wananchi kupata haki yao ya msingi. Nadhani si sahihi kwa watu waliojituma wenyewe kubebeshwa mizigo ya serikali, nakupongeza kwa kujitolea kusaidia kwa kutumia kipato chako binafsi kutatua matatizo ya serikali. SULUHISHO-BADILISHENI UTAWALA MJARIBU WENGINE MAANA WALIOPO HAWAONI KUWA ELIMU NI HAKI YA RAIA

Anonymous said...

jamani hii ni shule ya kulipia au ni ya serikali?? Mbona miaka ya zamani mtu ukichaguliwa kuendelea na sekondari serikali inagharimu kila kitu na unachotakiwa kuchangia ni kidogo sana?? Lini mambo haya ya kulipa malaki kwa wananchi wa kawaida yameanza. Hembu tufahamisheni jamani wengine tuliondoka enzi za nyerere. KILA KITU NI FREE ILI MRADI UMECHIMBUKA NA UKAFAULU NA KUCHAGULIWA SHULE ZA SERIKALI.