ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 23, 2012

MATUKIO KATIKA PICHA MCHEZO WA STARS ILIVYOICHAPA ZAMBIA 1-0

Hii ni Nduki aliyoipiga Mrisho Ngassa na kuja wavuni moja kwa moja huku kipa wa timu ya Zambia Chipolopolo, Danny Munyao akiwa hana la kufanya na kuishia kuutizama ukijaa wavuni
Mshambuliaji wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya Zambia katika mchezo wa kirafiki uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda goli 1-0.
Hamis Mcha (7) akiendelea kuwapa kazi mabeki wa timu ya Zambia.
Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akiingia kwenye lango la timu ya Taifa Stas,huku beki wa Stars,Aggrey Moris akijiandaa kukabiliana nae.
Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akijipinda kumramba chenga Kiungo wa Stars, Salum Abubakar, kutaka kumtoka wakati wa Mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar. Katika mchezo huo, Taifa stars imeibuka ushindi wa bao 1-0, lililotiwa kimiani na Mshambuliaji machachaari, 'Kisirani' Mrisho Ngassa katika dakika ya 45 ya kipindi ca kwanza. 
Mashabiki wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars wakiwa na nyuso za furaha baada ya Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Zambia.

No comments: