Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mh. Eugean Mwaiposa (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Dar es Salaam mapema leo asubuhi wakati wa kutangaza uzinduzi wa Mkakati wake wa kuwainua kiuchumi wananchi wa Jimbo lake la Ukonga kupitia Mradi aliouanzisha ujulikanao kama "JAMII NA MAENDELEO UKONGA", ambapo amefanikiwa kuvikusanya vikundi vya wafanyabiashara ndogo ndogo waliopo kwenye Jimbo la Ukonga na kwa umoja huo pia ameanzisha Saccos ya Jimbo itakayowawezesha wafanyabiashara hao kupata mikopo ya kuendeleza biashara zao inayotambulika kwa jila la UKONGA VICOBA SACCOS LTD (UVICOSA). Kulia ni Mwenyekiti wa Muda wa Saccos hiyo, Bi. Adivela Ruge.
Katibu wa Ukonga Vicoba Sacos (UVICOSA), Bi. Mary Katobes (kushoto) akiongea wakati wa kuwahamasisha wananchi wa jimbo la Ukonga (kupitia vyombo vya habari) kujitokeza kwa wingi kujiunga na Sacos yao hiyo.
Meneja wa Mradi wa Jamii na Maendeleo Ukonga, Suzan Miseda akiongea katika mkutano huo na Waandishi wa Habari.
No comments:
Post a Comment