Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe akiangua kilio wakati akimsikiliza mtoto Diana Haule (11) mkazi wa Shauri moyo wilaya ya Ludewa ambae amelazwa katika wodi namba 6 akitibiwa majeraha ya moto ambayo ameyapata baada ya kuangukia motoni kutokana na ugonjwa wa kifafa unaomsumbua
Mbunge Filikunjombe akitazama mikoni ya mtoto Diana ambayo imeungua kwa moto kushoto ni mama mzazi wa mtoto huyo
Mbunge wa jimbo la Ludewa na familia yake wakiwajulia hali wagonjwa kama ilivyoutaratibu wake wa kila sikukuu kula na wagonjwa wa zanahati na Hospitali mbali mbali jimboni mwake .
Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe leo amejikuta akibubujikwa na machozi baada ya kutembelea wodi la majeraha ya moto katika Hositali ya Misheni Rugalawa na kukutana na mtoto Diana Haule (11) mkazi wa Shaurimoyo ambae ameungua kwa moto mwili wake na kuimbiwa wimbo maalum uliomfanya kutokwa na machozi.
Mbunge huyo akiwa na familia yake ya mke na watoto wawili pamoja na viongozi wa CCM wilaya ya Ludewa aliofika katika wodi namba 6 ambalo mtoto huyo amelazwa aliokelewa kwa wimbo maalum kutoka kwa mtoto huyo ambao ulikuwa ukimsifia mbunge huyo na wakati akiusikiliza na kumtazama mtoto huyo mbunge huyo alianza kutokwa na machozi na kulazimika kuwaomba watu ambao alikuwa ameongozana nao kutoka nje ya chumba hicho na kumuacha yeye na mtoto huyo na watu wachache.
katika wimbo huo mtoto huyo alikuwa akieleza jinsi ambavyo ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na tatizo na ugonjwa wa kifafa linalomsumbua na Pamoja na kumpongeza mbunge kwa kufika kumjulia ari.
Kutokana na wimbo huo mbunge Filikunjombe alijikuta akiinamisha kichwa chini na kuanza kutokwa na machozi huku akiendelea kumsikiliza mtoto huyo akiendelea kuimba.
Hata hivyo mbali ya kueleza kusikitishwa na tatizo la mtoto huyo bado mbunge huyo aliahidi kuendelea kumsaidia mtoto huyo ikiwa ni Pamoja na kuisaidia Hositali hiyo zaidi .
Mtoto huyo anadaiwa kuungua kwa moto toka mwezi wa 9 mwaka huu baada ya kuangukia motoni wakati akiwa na mamake mdogo jikoni akiendelea kuandaa chakula .
Wakati huo huo mbunge Filikunjombe amekabidhi misaada mbali mbali katika Hospitali hiyo yakiwemo mashuka kwa wagonjwa wodi zaidi ya 80 na kandambili pamoja na kutoka msaada wa chakula vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2
No comments:
Post a Comment