ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 22, 2012

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA ASHIRIKI IBADA MAALUM NA JUMUIYA YA SHREE SANATAN DHARMA SABHA KULIOMBEA TAIFA AMANI.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahindu Tanzania Bw. Ramesha Patel akimpokea na kumtambulisha mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati alipowasili kwenye msikiti mkuu wa Dhehebu hilo ulioko jijini Dar es Salaam kwa shughuli maalum ya kuliombea taifa Amani.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akilakiwa na kuvishwa shada la maua.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiingia katika msikiti wa dhehebu la Wahindu kuhudhuria ibada maalum ya kuliombea taifa Amani.
Waendesha Ibada maalum kutoka India katika moja ya hatua za ibada hiyo wakimpa baraka za namna ya pekee Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akishiriki kuomba dua na waumini wa dhehebu hilo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa katika hatua nyingine ya ibada hiyo akizungushwa ndani ya msikiti huo.
Waumini wa dhehebu la Hindu wakiwa wamekusanyika katika sehemu maalum ya kufanyia ibada.
Ibada ikendelea kwa namna ya kipekee.
Baadhi waumini wakifuatilia ibada maalum.
Kwa picha zaidi bofya read more

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa na Mwenyekitiki wa Jumuiya ya Wahindu Bw. Ramesh Patel (kulia) na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Bw. Rajesh Mistry.
Pichani Juu na Chini watoto kwa wakubwa wakicheza ngoma za asili ya Hindu kwenye Ibada hiyo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akioneka kufurahishwa na ngoma hizo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wahindu ya Shreen Sanatan Dharma Sabha Bw. Rajesh Mistry akimkaribisha mwenyekiti wa jumuiya hiyo kuzungumza maneno machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
Bw. Ramesh Patel akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wanajumuiya hiyo wakati wa Ibada maalum ya kuliombea Taifa Amani.
Pichani Juu na Chini ni Mstahiki Meya akivishwa Ua na vazi la heshima kutawazwa kuwa mmoja wanajumuiya ya Hindu.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na wanajumuiya ya Hindu ambapo amewashukuru kwa kumkaribisha kuungana nao katika Ibada hiyo maalum na kuwataka kuendelea kuwa na mshikamano na jamii nyingine pamoja na Serikali.
Mstahiki Meya ametumia fursa hiyo kuwataka wanajamii hiyo pale wanapokwama au kukwazwa kibiashara katika manispaa ya Ilala kwa jambo wanaloona linaweza kutatuliwa wasisite kuwaona viongozi wao na kuwaambia viongozi wao wasisite kumuona yeye moja kwa moja ili watafute ufumbuzi kwa manufaa ya Manispaa na jiji kwa ujumla. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Ramesh Patel.
Igizo lililoonyeshwa baada ya kumalizika kwa Ibada hiyo.
Kiongozi wa kikundi cha maigizo akitambulisha washiriki wa igizo hilo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jery Silaa katika picha ya pamoja na wanakikundi cha ngoma za asili ya Hindu.
Picha Juu na Chini ni baadhi ya Waumini wa dhehebu ya Hindu waliohudhuria Ibada Maalum ya kuliombea Taifa Amani.

No comments: