Siku chache baada ya kukamilisha kushoot kichupa cha ngom ayake mpya ya 'Sorry' nyota kutoka nyumba ya vipaji nchini (THT) Barnaba Boy amesema ni upumbavu kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini kushoot video za muziki wao kutoka maeneo nje ya nchi.
Katika mahojiano maalum aliyoyafanya na teentz.com mapema leo Barnaba amesema kuwa, wakati mwingine inaweza isiwe jambo baya lakinikwake anaona ni upumbavu kufanya hivyo wakati nchi hii y akambarage imebarikiwa kuwa na vitu kibao vya kuvutia ambavyo vinaweza kupamba video ya wimbo husika.
"Hivi sasa naona watu wengi wanakimbilia kufanya video nje, si mbaya lakini binafsi siwezi fanya jambo hilo kwa kuwa naipenda nchi yangu na natamani kuendelea kuitangaza kila siku soo nahisi ni jambo bora kufanya video zangu hapa,bongo kwa kutumia warembo wa hapa na huo ndiyo uamuzi wangu ambao nahisi sitaubadilisha kamwe" alisema
Stori na Dismas Ten
No comments:
Post a Comment