ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 10, 2012

SHEREHE YA MIAKA 7 YA THT FUNIKA BOVU NDANI YA DAR LIVE

Wapenzi wa burudani wakifurahia shangwe wakati wa sherehe hizo.
Mzee Yusuf na vijana wake wakipagawisha stejini.
Mwanadada kutoka THT akionyesha swagga zake jukwaani.
Vijana wa THT wakiwasha moto wakati wa sherehe yao ya kutimiza miaka 7 ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Kwa picha zaidi bofya read more
Dancer wa THT akionyesha machejo jukwaani.
DJ Bulla kutoka Clouds FM akifanya vitu vyake.
Queen Darleen akiwarusha mashabiki.
Msanii Godzilla akiwapa raha mashabiki wake.
Dogo Aslay na Bi. Cheka wakikamua.
Dogo Aslay akiwadatisha mashabiki.
Ommy Dimpoz akiimba na mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live.
Mashabiki wakiinua mikono juu kuonyesha walivyokubali burudani zilizokuwa zikiendelea ndani ya Dar Live.
...Burudani zikiwa zimepamba moto.
Nyomi iliyohudhuria sherehe hizo.
Rachel akiwapagawisha mashabiki wake.
Juma Mataluma akifanya mambo.
Shilole na kundi lake wakilishambulia jukwaa la Dar Live.
...Shilole akizidi kuapagawisha.
...Mpaka chini.
Shetta akiwapa raha mashabiki.
Shangwe zikizidi kukolea ndani ya Dar Live.

WASANII wa nyumba ya vipaji, Tanzania House of Tallent ‘THT’ usiku wa kuamkia leo waliangusha bonge la pati ndani ya Ukumbi wa Dar live uliopo Mabagala jijini Dar kusherehekea miaka 7 ya kuanzishwa kundi hilo la kukuza vipaji. Katika pati hiyo wasanii mbalimbali wa muziki walitoa burudani hasa wasanii wenyewe wa THT. Pichani juu ni baadhi ya matukio yaliyojili ukumbini hapo.
(PICHA : RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA / GPL )

No comments: