Tuesday, December 25, 2012

SKYLIGHT BAND YANUKISHA MKESHA WA X-MASS KATIKA UKUMBI WA THAI VILLAGE JIJINI DAR


Warembo wenye asili ya Asia wakitoa burudani wakati wa mkesha wa X-MASS na SKYLIGHT BAND katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Mmoja wa warembo hao anatoa huduma ya kuuza vinywaji katika ukumbi huo nae akaona aonyesha kipaji chake kwa mashabiki wa Bendi hiyo na kweli anaweza.
Shine Bright like Diamond...Beautiful like a Diamond in the Sky.........Mmoja wa Shabiki wa SKYLIGHT Band mwenye asili ya Asia akipiga Kolabo na Aneth Kushaba AK47 kwenye mkesha wa X-MASS usiku wa kuamkia leo katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam.
Aneth Kushaba AK47 akiongoza safu ya vijana wa SKYLIGHT BAND Joniko Flower na Sony Masamba (kulia) kushambilia jukwaa wakati wa mkesha wa X-MASS Thai village jijini Dar.
Ghafla Jukwaa lilivamiwa na msanii wa Bongo Flava Beka aliyepanda Jukwaani kusindikiza usiku wa mkesha wa X-MASS sambamba na Sam Machozi a.k.a Sam Mapenzi (kulia).
Baadhi ya Mashabiki wa SKYLIGHT BAND wakionekana kulipuka kwa burudani ya msanii Beka akisindikizwa na Sam Machozi. Kwa mbali anaonekana Super star Sinta a.k.a JLO wa Bongo (mwenye Sketi ya pundamilia) akisakata rhumba.
kwa picha zaidi bofya read more
SKYLIGHT BAND wakiwajibika jukwaani.
Baadhi ya mashabiki wa SKYLIGHT BAND wakijinafasi kwa raha zao kwenye dancing floor.
Twende kazi....hapo chacha.
Carolina Mama njoo tucheze........ ni moja ya Hit Song ya SKYLIGHT Band ukiisikii hutotamani kukaa chini.
Umeshawahi kuona Pedesheee wa Kike??? basi huyo hapo pichani ni Mrembo Eshe Mushi akitunza pesa Wasanii wa SKYLIGHT BAND mpaka wa piga vyombo...Chezea toto la kichaga weweeee.
Aneth Kushaba AK 47 katika hisia kali.
Surprise nyingine ya Msanii Amini sambamba na Beka walitoa sapoti ya kutosha kwa SKYLIGHT BAND kuongeza vionjo.
Wadau wakipata Ukodak nao waliohudhuria.
Baadhi ya Mabaunsa wanaohakikisha Amani na usalama unakuwepo katika ukumbi huo kwa mashabiki wa Band hiyo. Ukileta fujo lazima ukae chini mwenyewe.

No comments: