ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 23, 2012

TAHADHARI YA VIPEPERUSHI MITAANI

Asalamu Alaykum kumesambazwa vipeperushi mitaani na taarifa katika wall mbali mbali za facebook za kuwahamasisha watu waunge mkono harakati za kutaka kuachiwa kwa maamiri wa Jumuiya ya Uamsho waliopo rumande kabla ya sherehe za Krismass, na inaelezwa kuwa chanzo au source ya kauli hiyo ni Msikiti Jibril, taarifa hizo zimeanza kusambazwa tokea Ijumaa wiki hii, nimefuatilia kwa karibu sana suala hilo lakini leo ndio nimewapata wahusika wakuu wa Msikiti wa Jibril na viongozi wa taasisi za kiislamu mbali mbali wakiwemo wa Uamsho wote wamesema taarifa hizo hawajatoa wao na wala hawahusiki na harakati yoyote kuhusiana na jambo hilo kwani viongozi wa Uamsho wamefikishwa mahakamani kwa hivyo wache sheria ifuate mkondo wake kwa mujibu wa sheria. kuanza kuingilia mahakama sasa hivi ni kosa kisheria na hivyo basi nawaombeni ndugu zangu wazanzibari msishabikie masuala kama hayo kwa wakati huu muhimu ambapo kuna mambo muhimu yanaikabili nchi na watu wakianza kuhamasishana watakuwa wamechokozwa na wamechokozeka kitu ambacho kinaweza kusababisha khatari kubwa huko mbele yetu kila mmoja na mtazamo na upokeaji wa taarifa kama hizi ambazo mwisho wake zinaweza kuhamasisha umma kuingia mitaani na kufanya fujo na kusababisha uvunjifu wa amani ambao hauna tija kwetu wala kwa taifa letu. Hilo ni ombi langu. Kuweni wavumilivu na msikubali kushawishiwa kwa aina yoyote ile ambayo haipo kisheria waliowekwa ndani wamewekwa kwa taratibu za kimahakama na watatolewa kwa taratibu hizo hizo za kimahakama hakuna haja ya kulazimisha kitu ambacho kitaleta madhara.

No comments: