ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 7, 2012

TALII TANZANIA KWA SIKU 14


Kampuni ya Lakeland Africa ya jiji Dar es Salaam imeandaa safari ya kutembelea hifadhi za taifa na makumbusho ya taifa ili kutoa fursa kwa Watanzania kusherehekea msimu huu wa Krismas na Mwaka mpya.
Watanzania wanahamasishwa  kujitokeza kushiriki katika safari hiyo ya kitalii ya siku 14 itakayoanza jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu hadi Desemba 27 mwaka huu. “Kwako mtanzania sasa inawezekana kujua Tanzania yako, si lazima kuwa mzungu kuwa mtalii wa ndani”
Safari hii itaanzia Dar es Salaam, na kupita katika hifadhi za Sadan, Pangani, Lushoto, Tarangire, Ziwa Manyara, Ngorongoro Crater, Hifadhi ya Serengeti na itahitimishwa Butiama kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Safari hii itatumia magari ya kisasa makubwa yenye uwezo wa kubebe watalii 24 na kutoa nafasi kutumia vifaa vya umeme (laptop, simu, kamera) kwa kila mtalii kuwa na soketi yake. Magari ambayo yamekuwa yakitumiwa na makampuni ya utalii katika nchi za ulaya sasa kutumika Tanzania pia.
Gharama za safari hii zinajumuisha chakula, malazi, usafiri, tozo za kuingia hifadhini na tiketi ya ndege kutoka Mwanza kurudi Nyumbani.
Kwa mawasiliano na Lakeland Africa
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi yako’

No comments: