MSHIKEMSHIKE wa aina yake uliibuka usiku wa kuamkia leo ndani ya Ukumbi wa Burudani wa Taifa wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wasanii 20 wanaowania gari katika shindano la The Mic King walipotoana jasho.
Shindano hilo ambalo lilikuwa likirushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha DTV cha lilikuwa na mvutano wa aina yake kutokana na vijana hao kuonyeshana vipaji vya hali ya juu.
Majaji Abdallah Mrisho, DJ Dilinga na Ally Baucha walikuwa na kazi kubwa ya kuwasimamia vijana hao kutokana na upinzani waliouonyesha.
Shoo za wakali wa Bongo Fleva zilitawala ukumbini hapo zikiwahusisha wasanii waliopelekana puta. Hao walikuwa ni Bob Junior, Suma Mnazareth, Chid Benz, Joh Makini, Dogo Aslay, Tunda Man, PNC, Dogo na Bi Cheka.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL)
No comments:
Post a Comment