BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Jumapili iliyopita ilionyesha kuwa wao ni magwiji wa muziki hapa nchini baada ya kudondosha burudani ya nguvu na kusababisha mashabiki waliofurika ndani ya ukumbi wa Taifa wa burudani Dar Live kupagawa.
‘Watoto’ hao wa Asha Baraka walivamia jukwaa la kisasa la ukumbi huo majira ya saa 3.30 usiku mara baada ya wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya kumaliza kukamua ambapo iliporomosha burudani mfululizo huku wanenguaji wao wakionyesha umahiri mkubwa na kuwafanya mashabiki waserebuke bila kuchoka.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL)









No comments:
Post a Comment