Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (kulia) akimkabidhi mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Waendesha Pikipiki mkoa wa Mwanza Makoye Bunoro Shilingi 50,000/= kwa ajili ya kuweka mafuta katika pikipiki za kitengo cha Polisi jamii pale wanapoenda kupambana na wahalifu.Umoja huo unawasaidia waendesha pikipiki 2034 kupata leseni na mafunzo yaliyotolewa na Chuo cha VETA kwa gharama naafuu.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (kulia) akiongea jambo hivi karibuni na viongozi wa umoja wa wapanda pikipiki wa mkoa wa Mwanza (hawapo pichani) alipowatembelea ofisini kwao eneo la Mlangommoja ili kuona shughuli zinazofanywa na umoja huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja huo Makoye Bunoro.
Mdhibiti wa mali za chama ch Umoja wa wapanda Pikipiki wa Mkoa wa Mwanza Faraji Abdalah akimwelezea Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (kulia) jinsi umoja huo ulivyoweza kuunda kitengo cha polisi jamii ambacho kinashirikiana na Jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja huo Makoye Bunoro.
Mwenyekiti wa Umoja wa wapanda pikipiki wa mkoa wa Mwanza Makoye Bunoro (kushoto) akimweleza Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi jinsi wapanda pikipiki wanavyohitaji kupata mafunzo na mikopo ya kununua pikipiki kutoka Serikalini ili waweze kujiajiri wenyewe na hivyo kujikwamua kiuchumi. (Picha na Anna Nkinda – Maelezo).
Na Anna Nkinda – Maelezo, Mwanza
No comments:
Post a Comment