Advertisements

Thursday, December 20, 2012

U.S.A MISS UNIVERSE OLIVIA CULPO AWABWAGA WALIMBWENDE WENZAKE NA KUJINYAKULIA TAJI HUKU AKISHINDWA KUAMINI KAMA KWELI ALISTAHILI KUSHINDA TAJI HILO.

Miss Universe 2011 Laila Lopes wa Angola akimvisha taji  Olivia Culpo baada ya kushinda Miss Universe 2012, mashindano haya ya lifanyika Las Vegas. Mashindano ya Miss Universe yalishirikisha walimbwende 89 na Olivia Culpo wa U.S.A kuibuka kidedea wa kinyanganyiro hicho. Olivia Culpo ana miaka 20 na ni mwanafunzi wa Boston University sophomore. Tanzania katika mashindano hayo tuliwakilishwa na Winfrida Dominic lakini hakubaatika kuingia top 15 lakini bado tunampongeza kwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi yetu.
Miss Universe 2012 Olivia Culpo wa U.S.A akindwa kuamini kama ameshinda kutokana na ushindani uliokuwepo katika mashindano hayo ya mwaka yaliyowashirikisha washiriki 89 kutoka nchi mbali mbali duniani.
Olivia Culpo Miss Universe 2012 baada ya kutangazwa mshindi wa mashindano hayo yaliyofanyika Las Vegas, Devada.
Miss Philippines Janine Tugonon akimpongeza Olivia Culpo baada ya kutanganzwa Miss Universe 2012
Hawa ndiyo waliongia tano bora na ndipo akapatikana mshindi wa taji hilo la Miss Universe 2012 Olivia Culpo wa U.S.A.

No comments: