ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 10, 2012

Vimini sasa marufuku vyuo vya KKKT

Na Yusuph Mussa, Lushoto

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo jijini Arusha, Profesa Joseph Parsalaw, amesema kuqanzia sasa ni marukufu kwa wanawake wanaosoma katika vyuo vikuu vyote na vile vishiriki vinavyomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kuvaa suruali za kubana au vimini.

Prof. Parsalaw aliyasema hayo juzi katika mahafali ya tatu ya
Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), kilichopo Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga na kusisitiza kuwa, lengo ni kutoa wahitimu ambao watakubalika kwenye jamii kwa matendo yao pamoja na uvaaji wao.
“Chuo Kikuu cha Tumaini kipo mstari wa mbele kuwahimiza wanafunzi na wafanyakazi kuzingatia maadili yanayokubalika kwenye jamii ya Kitanzania.

“Hivi sasa katika vyuo vyote vishiriki, tumeweka bayana aina ya mavazi ambayo yanastahili kuvaliwa na vijana ili kudumisha heshima na maadili mema,” alisema Prof. Parsalaw.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha SEKOMU, Mchungaji Dkt. Anneth Munga, alisema chuo hicho ambacho pia kinatoa elimu maalumu, kitaendelea kuongeza mahitaji ya jamii.

Aliwataka wanataaluma ambao ni wahitimu katika mahafali hayo, kuwa mabalozi wazuri katika maeneo ya kazi ili jamii ijiridhishe kama wametoka katika chuo cha kanisa, kupata upako wa Mungu,
kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kuwanyenyekea watu.

Dkt. Munga aliwataka wasomi hao kukitangaza chuo hicho kwa mema, kuwa na moyo wa kuwakumbuka waliowashika mkono
kwa mara ya kwanza, kupata mwanga wa maisha na kuweza kuonekana mbele ya jamii.

Majira

1 comment:

Anonymous said...

I was just qurious whether this is Biblical, or something else. If it is, why missionaries who introduced Christianity in Africa wore shorts, mini-skirts, and other lighter dresses to comply with high tropical temperatures? Will the dress code make our colleges competative in science and technology? Why western students who wear tight jeans and mini-skirts are inventers of facebook, twitter,apple, space technologies, drones, internet etc while the entire world is dancing their music. Why Tanzanian engineering students who are reqiured to maintain dress code, as suggested by kkkt, can neither make a sewing niddle, nor transport corn from Rukwa to extremely poor parts of the country?