Christopher Katongo a.k.a Chris katongo akiwa na tunzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika wa BBC Mwaka 2012
Mshambuliaji Christopher Katongo ambaye juzi alitwaa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika wa BBC Mwaka 2012 ni miongoni mwa nyota wa mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) watakaotua nchini leo jioni kujiandaa na mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi, imefahamika.
Alisema msafara wa timu hiyo utakuwa na wachezaji 24 na viongozi nane, akiwamo kocha aliyeipa timu hiyo ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Gabon, Mholanzi Herve Renard.
Mbili na Katongo ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo, nyota wengine watakaoambatana na timu hiyo ni Stopilla Sunzu ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mwaka 2012 na pia Given Singuluma, mfungaji bora wa fainali za kwanza za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
Wengine ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Wengine ni Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Roderick Kabwe na Salulani Phiri.
Osiah alisema kuwa kiingilio cha chini katika mechi hiyo itakayoanza saa 10:00 jioni kitakuwa Sh. 5,000 wakati cha juu kitakuwa Sh. 30,000.
SAMATTA, ULIMWENGU
Osiah alisema kuwa washambuliaji nyota wa Stars, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao walishindwa kujiunga na wenzao katika mazoezi ya Stars kutokana na majeraha waliyoyapata wakiwa na klabu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanaendelea vyema na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhumbili.
“Timu yetu inaendelea vizuri na maandalizi lakini Samatta na Ulimwengu bado wanaendelea na matibabu Muhimbili, leo (jana) kocha (Kim) Poulsen alienda kuwajulia hali,” alisema Osiah.
“Kamati ya Utendaji ya TFF imeamua kuwalipia gharama zote za matibabu ingawa taratibu za FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa) zinataka wachezaji wanaoumia kwenye klabu watibiwe na klabu zao,” alisema.
“Lakini tumeamua kuwalipia ili kuendelea kuwapa moyo wa kuitumikia nchi yao.”
Taifa Stars imekuwa kambini tangu Desemba 12 kujiandaa kwa mechi hiyo hiyo dhidi ya Zambia.
MASHAUZI, NATURE
Katika hatua nyingine, wadhamini wa Taifa Stars, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yao ya Kilimanjaro wamesema mechi dhidi ya Stars itatanguliwa na burudani itakayotolewa na wasanii kadhaa maarufu nchini, wakiwamo Chid Benz, Isha Mashauzi, Dogo Janja, Juma Nature, Tunda Man na Bi. Cheka.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Gorge Kavishe aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa wameamua kuandaa burudani hiyo itakayofanyika Ijumaa kwenye viwanja vya TTC Chang’ombe jijini Dar es Salaam ili kutoa hamasa kwa Watanzania kujitokeza kuishangilia Stars wakati wa mechi yao ya Jumamosi.
“Wasanii wengi maarufu wamekubali kuja kutoa burudani na siku hiyo (Ijumaa) wachezaji wote wa Stars watapanda jukwaani kuwasalimia mashabiki watakaofika kushuhudia tukio hilo la kuongeza hamasa kwa timu ya taifa,” alisema Kavishe.
CHANZO: NIPASHE
Christopher Katongo hii ilikuwa mwaka 2007 alipokuwa club ya Brøndby nchini Denrmark. Wadenish wanamkumbuka sana na stail yake ya sarakasi baada ya kufunga goli.
Christopher Katongo akiwa na Mette Jensen mmoja kati ya washabiki wake nchini Denmark
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah, alisema kuwa Katongo ambaye alitwaa Tuzo ya ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika baada ya kuwashinda kina Didier Drogba wa Shanghai Shenhua na Yaya Toure wa Manchester City, atatua na wenzake kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 11:00 jioni.Christopher Katongo akiwa na Mette Jensen mmoja kati ya washabiki wake nchini Denmark
Alisema msafara wa timu hiyo utakuwa na wachezaji 24 na viongozi nane, akiwamo kocha aliyeipa timu hiyo ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Gabon, Mholanzi Herve Renard.
Mbili na Katongo ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo, nyota wengine watakaoambatana na timu hiyo ni Stopilla Sunzu ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mwaka 2012 na pia Given Singuluma, mfungaji bora wa fainali za kwanza za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
Wengine ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Wengine ni Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Roderick Kabwe na Salulani Phiri.
Osiah alisema kuwa kiingilio cha chini katika mechi hiyo itakayoanza saa 10:00 jioni kitakuwa Sh. 5,000 wakati cha juu kitakuwa Sh. 30,000.
SAMATTA, ULIMWENGU
Osiah alisema kuwa washambuliaji nyota wa Stars, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao walishindwa kujiunga na wenzao katika mazoezi ya Stars kutokana na majeraha waliyoyapata wakiwa na klabu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanaendelea vyema na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhumbili.
“Timu yetu inaendelea vizuri na maandalizi lakini Samatta na Ulimwengu bado wanaendelea na matibabu Muhimbili, leo (jana) kocha (Kim) Poulsen alienda kuwajulia hali,” alisema Osiah.
“Kamati ya Utendaji ya TFF imeamua kuwalipia gharama zote za matibabu ingawa taratibu za FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa) zinataka wachezaji wanaoumia kwenye klabu watibiwe na klabu zao,” alisema.
“Lakini tumeamua kuwalipia ili kuendelea kuwapa moyo wa kuitumikia nchi yao.”
Taifa Stars imekuwa kambini tangu Desemba 12 kujiandaa kwa mechi hiyo hiyo dhidi ya Zambia.
MASHAUZI, NATURE
Katika hatua nyingine, wadhamini wa Taifa Stars, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yao ya Kilimanjaro wamesema mechi dhidi ya Stars itatanguliwa na burudani itakayotolewa na wasanii kadhaa maarufu nchini, wakiwamo Chid Benz, Isha Mashauzi, Dogo Janja, Juma Nature, Tunda Man na Bi. Cheka.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Gorge Kavishe aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa wameamua kuandaa burudani hiyo itakayofanyika Ijumaa kwenye viwanja vya TTC Chang’ombe jijini Dar es Salaam ili kutoa hamasa kwa Watanzania kujitokeza kuishangilia Stars wakati wa mechi yao ya Jumamosi.
“Wasanii wengi maarufu wamekubali kuja kutoa burudani na siku hiyo (Ijumaa) wachezaji wote wa Stars watapanda jukwaani kuwasalimia mashabiki watakaofika kushuhudia tukio hilo la kuongeza hamasa kwa timu ya taifa,” alisema Kavishe.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment