Na Eliasa Ally, Iringa
WANANCHI wa Wilaya ya Mufindi, mkoa wa Iringa, wamekumbwa na hofu kubwa baada ya mkulima, Clement Mkuvasa (45) kucharangwa kwa kukatwakatwa na shoka kichwani mara nne na watu wasiojulikana kufuatia kuhisiwa kuwa ni mchawi ambaye anaua watu katika Kijiji cha Mapogolo wilayani humo.
Baadhi ya wananchi wakizungumzia tukio hilo na gazeti hili wiki iliyopita walisema kuwa, Mkuvasa aliuawa siku ya pili ya Krismasi mwaka jana baada ya watu wasiojulikana kumvizia na kumcharanga kwa shoka kichwani majira ya mchana wakati akirudi nyumbani kwake kutoka kula siku kuu kwa majirani zake.
Wananchi hao walisema kuwa mauaji hayo yamewatia hofu kutokana na mtu waliyetekeleza mauaji hayo kujichukulia sheria mikononi bila hata kumfikisha mbele ya mikono ya sheria na kuonesha ushahidi wa makosa yake kama anao.
Leonald Mwakandale, mkazi wa Kijiji cha Mapogolo alipohojiwa na mwandishi wetu alisema kuwa serikali inatakiwa kuchukua hatua kali dhidi ya watu ambao wamehusika na mauaji hayo kwani marehemu Mkuvasa alikuwa ni mtu mzuri kijijini hapo.
Alisema kwa sasa wanashindwa kutembea nyakati za usiku na kuongeza kuwa hofu kubwa imewakumba zaidi wazee ambao hawajui hatima ya maisha yao kutokana na kupigwa na kuuawa na vijana kwa madai kuwa ni wachawi waonawaloga watu ili wasipate maendeleo au kuwaua kwa kulogwa.
Akizungmzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda alikiri kutokea kwa mauaji hayo siku ya pili ya Krisimasi Desemba 26, mwaka jana 7:00 jioni, akaongeza: “Marehemu alikatwa na shoka mara nne kichwani na watu wasiojulikana, ambao walimvamia na jeshi la polisi bado linawatafuta wahusika wa tukio hilo la mauaji .”

GPL
No comments:
Post a Comment