Serikali imeiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, kuchunguza na kusimamisha ujenzi wa kiwanda cha vinywaji vikali kwenye eneo la makazi huko Himo na kumtoza faini mwekezaji kwa kukiuka sheria na taratibu za Mipangomiji.
Barua ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Januari 23, mwaka huu inatoa maelekezo hayo yanayotaka mwekezaji wa kiwanda kwenye kiwanja namba 16 kilichoko kitalu F eneo la Himo mkoani Kilimanjaro kusitisha ujenzi huo.
Waraka hup ulioandikwa na Mkurugenzi wa Mipangomiji na Vijiji wa Wizara Linus Shao na kunakiliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo na kwa Mbunge wa Vunjo (TLP) , Augustine Mrema, iliitaka halmashauri kufuatilia na kusimamisha ujenzi huo.
“… kama kiwanda kimeanza kujengwa ahakikishe kuwa hakijengwi na kumtoza faini mwekezaji kwa kosa la kubadili matumizi ya ardhi bila kibali cha Mkurugenzi wa Mipangomiji ya mwaka 2007 …” ilisema sehemu ya barua hiyo.
Kiwanda hicho kwa mujibu wa barua hiyo kipo eneo la makazi na lililitengwa kwa ajili ya huduma za ibada na matumizi ya umma lakini kimebadilishwa matumizi ya ardhi bila idhini ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo.
Shao aliungana na wakazi wa Himo waliopinga ujenzi kwa maelezo kuwa maeneo ya viwanda hutengwa mbali na makazi kwa sababu matumizi yake hukinzana.
Awali Mrema aliandika barua wizarani kuwasilisha maoni ya wananchi waliopinga ujenzi wa kiwanda hicho kwa maelezo kuwa ni eneo la ibada, karibu na makazi ya watu na ujenzi ulifanyika kinyume na sheria.
Habari za ndani zilisema mwekezaji huyo ni wa kigogo jina linahifadhiwa na kwamba alijenga kwa kificho hadi wananchi walipogundua baada ya kuweka bango la kutangaza kuwa kinazalisha pombe kali na mvinyo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment