ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 4, 2013

HIVI NI 'ELIMU BORA' AMA 'BORA ELIMU?'

Hili ni darasa lenye nafuu kubwa katika shule ya msingi Chanjale Ludewa mkoa wa Njombe

Hili pia ni darasa la shule ya Msingi Chanjale Ludewa na hapa ujenzi wake umekamilika na limekuwa likitumika kwa zaidi ya miaka 7 sasa 

 Ubao wa darasa la tano katika shule hiyo, sasa hebu nikuulize wewe waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt Shukru Kawambwa hivi umepata kutembelea shule hizi za pembezoni ama uwaziri wako ni wa mjini pekee pia watanzania tujiulize hivi hapa ni elimu bora ama bora elimu?
Hiki ni choo cha kisasa cha wanafunzi ambacho kinatumika na wanafunzi wa wavulana na wasichana shule ya msingi Chanjale Ludewa

Picha na Francis Godwin

No comments: