ANGALIA LIVE NEWS
Tuesday, January 29, 2013
Jiji lasubiri tathmini magari yaliyoharibiwa Ubungo
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi, amesema anasubiri taarifa ya tathmini itakapomfikia ndipo uamuzi itafanyika wa nani atahusika na malipo ya hasara iliyotokea katika tukio la ukuta kuangukia magari zaidi ya 20, eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Akizungumza na NIPASHE jana, Kingobi alisema kwa sasa hawezi kutoa maelezo juu ya nani anahusika na fidia ya hasara mpaka taarifa ya tathmini itakapomfikia. “Hili suala bado linafanyiwa kazi, hivyo siwezi kusema lolote juu ya hilo mpaka nitakapopata taarifa ya tathmini ndipo tutawaeleza zaidi juu ya hilo,” alisema Kingobi.
Alisema kuwa, anashindwa kulitolea uamuzi suala hili kwa kuwa wakati tukio linatokea hakuwepo jijini, lakini anaendelea kulifanyia kazi na atalitolea maamuzi baada ya kupata taarifa ya tathmini ya hasara iliyotokea
“Mimi mwenyewe sikuwapo nilikuwa safari kidogo na sina muda mrefu tangu nirudi, hivyo nami nasubiri nipate ripoti kamili ndipo niweze kulitolea maelezo zaidi pamoja na maamuzi mengine yatafuata,” alisema.
Jengo lililokuwa likitumika kwa ajili ya maegesho ya magari ya watu binafsi katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT) liliporomoka majira ya alfajiri na kuangukia na kuharibu vibaya magari 23 na bajaj tatu pamoja na watu wawili kujeruhiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment