ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 9, 2013

Mahojiano na Mhe Balozi Mwanaidi Maajar Part 1



Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar akiwa na Mzee wa changamoto wetu, Mubelwa Bandio, katika mahojiano yaliofanyika Siku ya Jumanne January 8, 2013 ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington DC Nchini Marekani. (Video Camera na swahilivilla.blog)

Hii ni sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano kati ya JAMII PRODUCTION na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico (anayemaliza muda wake) Mhe. Mwanaidi S. Maajar
Katika sehemu ya kwanza anaeleza
1: Historia ya maisha yake (kwa ufupi)
2: Ilikuwaje akaingia katika fani ya sheria? Na ni nini alipanga kufanya kabla ya kuamua kuwa mwanasheria?
3: Ni vipi alipokea ombi la kuwa Balozi?
4: Ni changamoto zipi anazokutana nazo kwenye kazi yake ya ubalozi?
5: Ni vipi anabadili mawazo ya waMarekani wanaoiona Tanzania kama nchi isiyopiga hatua?
6: Anawashirikisha vipi viongozi wa Tanzania katika maendeleo anayoyaona Marekani?
7: Ipi nafasi ya mwanamke katika uongozi?
8: Anazungumzia vipi suala la viti maalum kwa wanawake?
9: Je! Tanzania ipo tayari kuwa na Rais mwanamke? Na Je! Tanzania ina wanawake ambao wanaweza kuwa rais wa nchi?

Na mengine mengi.
KARIBU UUNGANE NASI

1 comment:

Anonymous said...

Huyu balozi sio mchezo. I enjoy listening to her because she has her stuff together. Very Smart, articulate and good person. I wish her the best on her future endevours.