Mwananchama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi. Subira Kibiga akitoa maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Wengine ni wananchama wenzake Bi. Diana Mwiru (kushoto) na Bi. Asseny Muro.
Mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi. Asseny Muro akitoa maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa TGNP Bi. Mary Rusimbi na Mjumbe wa Bodi ya mtandao huo Prof. Ruth Meena.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi, akiongea katika mkutano na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) uliolenga kupata maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Wajumbe wengine wa Tume, Bi. Mary Kashonda na Bi. Salma Maulidi.
Baadhi ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika picha ya pamoja na Wanachama na viongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) mara baada ya mtandao huo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam).
(Picha na Omega S. Ngole, Principal Information Officer, Constitutional Review Commission (Tanzania) )
No comments:
Post a Comment