ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 4, 2013

Mancini, Balotelli wakunjana

Mchezaji wa Man City, Scott Sinclair akihamaki baada ya Mario Balotelli kumchezea rafu mbaya huku mchezaji mwenzake akiangalia
Kocha Roberto Mancini akimkwida fulana Mario Balotelli kitendo ambacho hakimfurahisha Balotelli na kilimfanya apandishe hasira
Kocha Roberto Mancini akiendelea kumkwida Mario Balotelli huku akifoka kwa hasira
Mmoja ya wafanyakazi wa Manchester City, Massimo Battara (wapili toka kushoto) akisaidiana na kocha msaidizi wa timu hiyo wakiingilia kati kuamlia ugovi.
Massimo Battara akimuondoa Balotelli uwanjani hapo huku kocha msaidizi akimdhibiti Roberto Mancini


Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliiambia Sky Sports: “Mancini akiwa na hasira alimfuata Balotelli na kumkunja fulan huku lengo likiwa ni kujaribu kumwangusha chini.

LONDON, England
AKITUHUMIWA kuporomoka kiwango, mshambuliaji wa Manchester City, Mario Balotelli na kocha wake, Roberto Mancini jana walitoleana uvivu na kutupiana maneno yaliyosababisha kukunjana mashati wakati wa mazoezi ya timu hiyo.
Bosi Mancini alionekana akimkunja fulana Balotelli jambo lililompandisha hasira mchezaji huyo kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, Carrington.
Balotelli (22), alionekana akiondolewa eneo la tukio na mmoja wa wafanyakazi wa klabu hiyo, Massimo Battara mara baada ya kutenganishwa.

Tukio hilo limewashtua mashabiki wa timu hiyo inayojiandaa na mechi ya Kombe la FA dhidi ya Watford.

Mancini alikasirishwa vikali kufuatia rafu mbaya aliyocheza Balotelli dhidi ya mchezaji mwenzake Scott Sinclair wakati wa mazoezi.
Hali hiyo ni wazi inaendelea kumweka kwenye wakati mgumu Balotelli, raia wa Italia ndani ya klabu hiyo.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliiambia Sky Sports: “Mancini akiwa na hasira alimfuata Balotelli na kumkunja fulan huku lengo likiwa ni kujaribu kumwangusha chini.

“Lakini ilionekana kana kwamba Mario ana nguvu zaidi na hivyo kushindwa kumwangusha chini. Kisha makocha wote wakakimbilia eneo la tukio kuwatenganisha, huku Mancini akionekana wazi kutotaka kutenganishwa.”

Baada ya tukio hilo, Balotelli alikwenda kwenye gari lake la kifahari, Bentley GT na kuondoka sehemu hiyo ya mazoezi. Hatima yake kuondoka Etihad sasa inaonekana kukolea baada ya tukio hilo.

Wakati Balotelli alipotolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Arsenal msimu uliopita, Mancini aliwahi kusema kwamba ulikuwa mwisho wake.

Baadaye, Mancini alisema: “Siwezi kuendelea kufanya kazi uwanjani na Mario. Kila wakati tunakuwa kwenye hatari ya kupoteza mchezaji mmoja kama ilivyotokea leo (jana).
Kisha akasema: “Imetosha. Kuna mechi sita na hatacheza, yuko kwenye adhabu.”
MWANANCHI.

No comments: