Mgeni rasmi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho akisalimiana na kipa wa Azam FC, Mwadini Ally katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba SC kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar uliochezwa usiku wa kuamkia leo. Azam ilishinda kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120.
Kikosi cha Simba
Kikosi cha Azam
Kipre Balou wa Azam kulia akiwania mpira wa juu na Abdallah Seseme wa Simba
Samir Hajji Nuhu wa Azam akiwatoka wachezaji wa Simba
Picha kwa hisani ya Bin Zubery Blog
Miraj Adam wa Simba akiuwahi mpira dhidi ya Hajji Nuhu wa Azam
Humphrey Mieno wa Azam aliyeenda hewani kuifungia bao la kwanza timu yake
Wachezaji wa Azam, Ibrahim Mwaipopo kushoto na Uhuru Suleiman kulia wakimdhibiti kiungo wa Simba SC, Ramadhani Singano 'Messi' katikati huku kocha wake Jamhuri Kihwelo 'Julio' kulia kabisa akishuhudia
Wachezaji wa Azam wakimpongeza Humphrey Mieno kufunga bao la kwanza
Paul Ngalema wa Simba akimdhibiti Uhuru Suleiman wa Azam FC
Ibrahim Mwaipopo anatoa pasi huku akiwa amebanwa na wachezaji wa Simba SC
Kipa wa Simba SC, William Mweta akiwa amedaka mbele ya mshambuliaji wa Azam, Brian Umony huku beki wake Paul Ngalema akiwa tayari kutoa msaada kulia
Seif Abdallah wa Azam akiwatoka mabeki wa Simba
Ramadhani Mkipalamoto akiwatoka mabeki wa Azam
Kipre Balou akimiliki mpira mbele ya Jonas Mkude wa Simba
Haruna Chanongo akitoa pasi kwa kichwa mbele ya Ibrahim Mwaipopo
Miraj Madenge wa Simba, akimiliki mpira mbele ya Himid Mao wa Azam
Himid ameosha mbele ya Madenge
Madenge akimpongeza Rashid Ismail kufunga bao la kwanza la Simba SC
Mwadini Ally amedaka mbele ya beki wake Himi Mao, huku Ramadhani Mkipalamoto akifukuzia
David Mwantika wa Azam akimdhibiti Mkipalamoto wa Simba SC
Samih Hajji Nuhu amempitia Mkipalamoto na mpira wake
Daktari wa Simba SC akimtoa nje beki Hassan Hatibu baada ya kuumia kiasi cha kushindwa kuendelea na mchezo
Mkipalamoto amemlamba chenga Himid Mao, anaondoka...
Lakini shuti lake lilidakwa na Mwadini...lilikuwa bao la wazi sana alikosa
Gaudence Mwaikimba akipiga mpira kichwa ambao ulitoka nje sentimita chache
Hatari langoni mwa Simba SC
Lakini salama...
Himid Mao akiwa ametoa mpira nje kupunguza kasi ya Haruna Chanongo wa Simba SC
Mwantika amezuia, anaanza kugeuka taratibu
Miraj Madenge akishangilia baada ya kuifungia Simba bao la pili
Kutoka kulia ni Hassan Khatibu na Rashid Ismail wakicheza na Miraj Madenge kumpongeza kwa kufunga bao la pili
Mkipalamoto akitafuta mbinu za kumtoka Mwantika
Hapa ni wakati Azam ikiwa nyuma kwa 2-1, tazama sura ya kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall ilivyokuwa
Brian Umony akiwa benchi baada ya kutolewa
Kipa wa Simba SC, William Mweta akigagaa mpira ukiwa nyavuni...ni baada ya mkwaju wa penalti wa Joackins Atudo kuipatia Azam bao la kusawazisha
Wachezaji wa Azam Seif Abdallah kulia na Humphrey Mieno kushoto wakiwa kwenye benchi baada ya kutolewa
Makocha wanne wa kigeni wa Azam wakiwapa mawaidha wachezaji wao kabla ya kuingia kumalizia dakika 30 za nyongeza
Kuna wakati ilibidi Stewart Hall aombe ushauri kwa mchezaji wake wa akiba, Luckson Kakolaki kushoto ambaye anamuambia cha kufanya, bila shaka ilikuwa ushauri mzuri na ndiyo maana timu ilishinda
Shujaa wa Azam, Malikqa Ndeule akiwa amebebwa juu juu
No comments:
Post a Comment