Na Wilbert Molandi
KOCHA Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ametamba kuwa kwa kushirikiana na kocha mpya klabuni hapo, Patrick Liewig na meneja wake, Moses Basena, watatengeneza timu bora yenye ushindani.
Liewig, raia wa Ufaransa, alitua nchini wiki iliyopita na kusaini mkataba wa miezi 18 kuifundisha timu hiyo. Wote kwa pamoja (Liewig, Basena na Julio) watashirikiana katika kufanya kazi.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Julio alisema Klabu ya Simba pekee ndiyo yenye makocha watatu wenye uwezo wa kimataifa ambao kila mmoja ana ufundi wake binafsi utakaokiimarisha kikosi chao kinachojiandaa na Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Uwepo wa Liewig, Basena na mimi utafanya kikosi chetu kiwe bora zaidi, wote ni makocha wenye uwezo wa kimataifa na mbinu tofauti ambazo kama wachezaji wetu wakizishika na kuzitumia ndani ya uwanja, ninaamini tutafanya vizuri kwenye ligi na mashindano mengine,” alisema Julio.

No comments:
Post a Comment