Kutokana na mahitaji ya muda mrefu ya watalii na watanzania,
kupata huduma ya kuwezeshwa kulipia vyumba vya mahoteli na huduma za kitalii
kwa njia ya mtandao kwa bei nafuu, kampuni ya Vinjari imeanzisha huduma hiyo
kwa kupitia tovuti yake ya www.vinjari.co.tz
Kwa kupitia mtandao wa Vinjari sasa mtu yeyote mwenye kadi
ya VISA (iliyowezeshwa kufanya manunuzi kwenye mtandao) na yule mwenye akaunti
ya M-Pesa (Tanzania) anaweza kulipia huduma hizo sasa kwa kupitia www.vinjari.co.tz. Huduma hii imetengenezwa kwa kuzingatia viwango vya
kimataifa na kuthibitishwa na taasisi
inayoidhinisha mitandao inayotoa huduma za malipo mbalimbali duniani.
Katika kuperuzi mtandao wa vinjari, mteja ataweza kuchagua
aina ya hoteli, mkoa anaotaka kwenda,tarehe anayotaka kwenda pamoja na kiasi
ambacho ana uwezo wa kulipia. Mtandao huu kwa sasa unatoa huduma katika mikoa
ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Pwani, Mbeya, Kigoma, Kagera
pamoja na Zanzibar.
Vinjari inawakaribisha watu wote katika ulimwengu wa
kiteknolojia unaorahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali popote ulipo. Pia
unaweza kufuatilia huduma za Vinjari kwa kupitia Facebook (www.facebook.com/vinjari) na Twitter
(https://twitter.com/VinjariTanzania).
No comments:
Post a Comment