
Mdau leo nimekuja na mada hii ya ni sababu zipi zinazopelekea watoto wengi wa kike kua karibu sana na baba zao kuliko mama hata wakati mwingine mtoto wa kike anaweza sababisha baba na mama kutoelewana nyumbani, mtoto anaweza kukosa kitu mama anakuja juu lakini baba anamtetea je wewe unafikiri sababu ni nini?
5 comments:
Ngoje nieleze kwa lugha rahisi. Mtoto wa kike kabla hajabalehe na kupata rafiki wa kiume, baba yake huchukua nafasi ya rafiki yake wa kiume. Mtoto wa kike hujifunza mengi kuhusu wanaume kutoka kwa baba yake. Laki, akikua na kupata rafiki wa kiume urafiki na baba yake hupungua. Huendelea kujifunza toka kwa huyo rafiki wa kiume hadi anapoolewa.
kitu kingine mtoto wa kike humtambua baba yake kama ndio mwanaume pekee ambaye hataweza kuja kumuumiza moyoni siku zote baba humpa mapenzi ya kweli, mtoto wa kike ataumizwa na wanaume wengine awe boyfriend, mume lakini baba yake ndie pekee mwenye mapenzi nae ya kweli kwake kwangu mimi naona pia hii n sababu moja wapo ya mtoto wa kike kuwa karibu na baba yake
Hayo ndiyo matatizo nilyonayo mwenzenu kwakweli..napambana nayo hivo hivo..
girl always a little princess to a father. baba unamuona mtoto wako toka alipozaliwa hadi anapokua kua na uhusiano kati yako na yake unakua zaidi, likewise mtoto wa kiume na mama. hii gender issue ambayo jibu lake analijua muhumba.
Anonymous wa Jan 4, 2013 unamatatizo gani tena. Weka email yako nikuandikie :)
Post a Comment