Advertisements

Friday, January 18, 2013

Nyota Ndogo Atupiwa Lawama

Nyota_Ndogo_Getmziki.jpg (560×372)
Mwanamuziki wa nchini Kenya, Nyota Ndogo, amepata maswahiba makubwa ikiwa ndio kwaanza mwaka unaanza hasa baada ya kuibuka kwa mwanamuziki chipukizi ambaye anadai kuwa mwanadada huyu amemuibia wimbo yake.

Msanii huyu chipukizi ambaye anakwenda kwa jina Kachela Kroma, amesema nyimbo hiyo inabeba ujumbe wa amani ndani yake, na kwa kuthibitisha zaidi hili amesema kuwa, alirekodi kazi hii mwaka 2007 baada ya vurugu za uchaguzi mkuu wa nchini Kenya.

Msanii Nyota Ndogo hajaweza kupatikana kuzungumzia hili mpaka sasa ili kupata ukweli halisi wa inshu hii ambayo kiukweli, Kachela anamlaumu mtayarishaji muziki Jesse kutoka Ketebuk Music kwa kuvujisha kazi hii.

No comments: