MKAZI mmoja wa Kiwira, Rungwe mkoani Mbeya, Joseph Mwaenga (32) ambaye ni mwendesha pikipiki amenusurika kujilipua na kulipua kituo cha polisi mjini hapa akipinga vitendo vya uonevu vinavyofanywa na askari hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman amewaeleza waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa tukio hilo limetokea saa 5 usiku katika eneo la kituo hicho.
Alisema kuwa kijana huyo ambaye ni mwendesha bodaboda alifikishwa kituoni hapo baada ya kufanya vurugu katika kijiwe cha maegesho ya pikipiki na baada ya hapo alipokonywa pikipiki yake na wananchi na kuifikisha polisi.
Hata hivyo, baada ya kufikishwa kituoni hapo akiwa nje ya kituo alijimwagia mwilini petroli aliyokuwa nayo ndani ya dumu na kumwagia kituo cha polisi kisha kutoa kiberiti na kutaka kujilipua yeye na kituo hicho kabla ya kudhibitiwa na askari wa zamu.
Alisema kuwa hakuna madhara yaliyojitokeza kwa binadamu wala mali juu ya tukio hilo na mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
Chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment