MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ametoa kali ya mwaka baada ya kueleza kuwa, mara nyingi hapendi kuhudhuria kwenye misiba kwa kuogopa kulogwa.
Akiongea na mwandishi wa kipande hiki , msanii huyo alisema sehemu nyingi zenye mikusanyiko ya watu ndiko wale walozi wanakofanyia kazi yao ya kuwaloga watu ndiyo maana alikacha mazishi ya John Maganga, Mlopelo, Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
“Yaani mimi siku hizi sipendi kabisa kwenda kwenye mikusanyiko ya wasanii na watu wengi kwani huko ndiko tunamalizana hivihivi kwa kulogana. Japo vifo vya wenzangu vimeniuma sana lakini sina la kufanya ila nawaombea kwa Mungu,”alisema Baby Madaha.
1 comment:
namunga mkono na miguu na akili zangu zote kwa kauli yake aliyoitoa baby madaha, nikweli sehemu ya msiba/misiba na especially ikiwa inatugusa ya wenzetu au hata kama hatugusu lakini ni binadamu wenzetu tunabidi kwa mila zetu za kiitanzania tuhudhuriye lakini ikitokea kuna wanga wanatafuta kuwafanyia watu ubaya mtu unajiuliza mara mbili mbili hivi watu hawa wana nia gani hasa mtu unakwenda msibani unarogo mimi mama yangu mzazi kuna mtu kajidai kumuweka kakanga yake vizuri kasika kidogo huku kachomowa nyuzi kijanja za ile kanga bila ya sisi kujua na akaenda akafanya alivyo fanya mama hakukaa sana duniani akafa kifo cha ghafla na yule mwanamke akaja kuolewa na baba, najua utasema mengi na kusema uswahili imani potufu na yote yale na siku zake zimefika lakin jamani tutake tusitake uchawi upo na wanga wanakuja sana katika sherehe zetu bora baby madaha ajipumzikiye kwake na awaombe dua wasania wenzake walio kufa mungu anajua nia na imani yake na kuona wanaokwenda kwa masikoni hata hawana uchungu na wahusika kazi zao kupiga story na habari za umbeya na mpira na kuonyeshana mavazi walio vaa.
si afadhali ya baby madaha mtamshanga sana kwa kauli yake lakini mimi namuunga mkono, miguu na akili zangu zote kasema kweli na kuwa muwazi si mnafiki kama wenginewe.
mdau italy
Post a Comment