ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 23, 2013

Skylight Band yazidi kupasua anga za kimataifa katika muziki wa live Band jijini Dar

Aneth Kushanba AK47 akiongoza safu ya vijana wa SKYLIGHT Band kutoa burudani kwa mashabiki wake Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha maraha Thai Village Masaki Jijini Dar. Bendi hiyo inapiga hapo kila siku za Ijumaa kuanzia Saa 3 usiku.
Sura mpya ya SKYLIGHT Band binti mrembo mwenye kipaji cha aina yake na sauti ya kumtoa nyoka pangoni Salma Yusuf akitoa burudani kwenye ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar.
Mary Lukas akiimbia kwa hisia kali.
Kijana Sam Mapenzi (katikati), Aneth Kushaba AK47 na Joniko Flower wakiwa mzigoni.
Mzungu mmoja ambaye ni shabiki wa SKYLIGHT Band akimwaga mauno huko jasho likimtiririka samba samba na msanii Joniko Flower.
Mmoja wa wapiga vyombo wa Skylight Band akionyesha kipaji chake cha kusakata sebene.
Watu weeeeee mzungu noma......ilibidi watu waache kucheza na kumshangaa shabiki huyo wa kizungu aliyekuwa kivutio kwa wengi hata mkongo haingii ndani kwa mauno yake.
Pichani Juu na chini ni mashabiki wa Bendi hiyo wakijinafasi kwa raha zao.....Full kupagawa.....Chezea Skylight Band wewe...
Twende kazi..... Wera wera chapa ilale.......
kwa picha zaidi bofya read more

Ukawadia ule muda wa mduara na mambo yalikuwa kama hivi.....
Mwanamke nyonga hasa ukijaaliwa kuizungusha.
Mashabiki wa SKYLIGHT Band wakishow love.
Mwisho Mwampamba ndani ya nyumba.
Mdau Benjamin katika pozi na mtoto wa ukweli.
Mariam Nnauye na TID.
Mdau Benjamin(katikati) akishow love na marafiki.
Mdau wa Michezo kutoka Clouds Fm Shaffi Dauda (wa pili kushoto) akishow love na marafiki.
Mashabiki wa SKYLIGHT Band wakila bata katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita.
Kila siku mashabiki wapya wanazidi kumiminika.....
Prof. Jay sambamba na mshikaji wake Kiboya nao walikuwepo.
Wema Sepetu na Zamaradi Mketema wakiserebuka.
Mdau akaomba kupata ukodak na warembo hao.
Wadau wa SKYLIGHT BAND hawakukosa.

No comments: