Advertisements

Tuesday, January 15, 2013

TASWIRA MBALIMBALI ZA MKUTANO WA DK SLAA NA UFUNGUZI WA MATAWI MJINI MOSHI JANA

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa akipandisha bendera ya Chama kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la CHADEMA Classic lililoko katika kata ya Longuo Moshi Mjini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa akikata utepe wakati akizindua tawi la vijana wa CHADEMA la Aslam Garage Moshi Mjini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa akipokelewa na wananchi wa Mtaa wa Kibo ambapo alifungua matawi na ofisi ya Kata na baadae kufanya mkutano mkubwa katika viwanja vya Njoro Mjini Moshi.
Wananchi wakionesha ishara ya kujibu swali la Dk Slaa aliyewauliza wakazi hao wa Moshi Mjini ni nani ambaye kwa muda ule alikuwa tayari kujiunga na CHADEMA.
Kwa picha zaidi bofya read more
Wananchi wakigombania kununua kadi za uanachama wa chama hicho wakati wa mkutano.
Sehemu ya mahudhurio ya wananchi katika mkutano huo.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akihutubia.
Wakazi wa jimbo la Moshi Mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Njoro jana.

(PICHA ZOTE: DIXON BUSAGAGA WA GLOBU YA JAMII MOSHI NA ARUSHA255.BLOGSPOT.COM)

No comments: