Advertisements

Tuesday, January 22, 2013

Umeme wakatisha shughuli za baraza


Na Salma Said, Zanzibar

KIKAO cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea Chukwani Mjini Unguja kimelazimika kusitishwa kwa muda kutokana na hitilafu ya umeme iliyotokea katika ukumbi wa baraza hilo la wawakilishi hapo jana asubuhi.

Akitoa tangazo kwa wajumbe wa baraza hilo Spika wa Baraza hilo, Pandu Ameir Kificho aliwaambia wajumbe kwamba kutokana na khitilafu hiyo kikao hicho anakiakhirisha hadi jioni ili kutoa fursa kwa mafundi wa umeme kuja kufanya matengenezo katika ukumbi huo.

Spika Kificho alisema licha ya kuwachwa jenereta na kuendelea na shughuli za baraza hilo lakini kutokana na ukumbwa na mahitaji makubwa ya umeme katika ukumbi huo majenereta hayo hayana uwezo wa kumaliza shughuli zima ya vikao vya baraza hilo na hivyo wanalazimika kuwapisha mafundi kuendelea na kazi ya matengenezo.

“Waheshimiwa wajumbe kutokana na khitolafu ya umeme katika ukumbi wetu huu naomba kuakhirisha kikao hiki hadi hapo jioni ili tutoe nafasi kwa mafundi waliofika hapa kuja kututengenezea umeme kwa sababu jenereta lililowachwa haliwezi kutumalizia shughuli yetu hii muhimu” alisema Spika.

Hata hivyo wajumbe wa baraza la wawakilishi walionekana kutoka wakiwa na furaha baada ya kusikia kikao hicho kimeakhirishwa na waliendelea jioni baada ya matengenezo hayo kufanywa na wataalamu na mafundi kutoka Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO).

Ukumbi wa baraza la wawakilishi umejengwa kwa ufadhili wa Sheikh Ali Yussuf wa Saudi Arabia na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lakini ukumbi huo umekuwa na khitilafu za mara kwa mara katika mitambo yake ya umeme, vipaza sauti na hata baadhi ya jengi hilo limekuwa kilivuja maji.

Afisa mmoja wa baraza hilo aliliambia Mwananchi kwamba ujenzi wa jengo hilo haukuwa mzuri aktika ramani yake kutokana na kuwa mafunzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) wameshindwa kuona njia na paipu za kupitishia maji machafu na hivyo kuvuja kwa maji kumeshindikana licha ya juhudi kadhaa kufanywa na wataalamu wa ZAWA kujaribu kutaka kufanya marekebisho njia hizo za maji ndani ya jengo hilo.

“Jengo hili tokea limejengwa kuna matatizo mengi si unakumbuka wawakkilishi wakilalamikia vipaza sauti havisikiki na sasa umeme una matatizo lakini pia kuna tatizo la maji hapa wamekuja wafundi na wataalamu wengi sana lakini wameshindwa kuona paipi hawajui zimefukiwa au zimezamishwa wapi kwa hivyo maji yanamwagika na hayana pa kutokea na wale waliojenga wala hawapo sasa sijui tena serikali itafanyaje” alisema Afisa mmoja wa baraza la wawakilishi.


mwisho

waliokataa sensa wameitia hasara serikali


SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kitendo cha baadhi ya wananchi kususia sensa kilisababisha serikali kuingia gharama kubwa katika kuendelea kuhamasisha umma kukubali zoezi hilo kwa maendeleo ya Taifa
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar,  Omar Yusuf Mzee ameyasema hayo alipokuwa akijibu suala la msingi katika ukumbi wa baraza la wawakilishi  linaloendelea huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanziba lililoulizwa na mwakilishi wa Kiwani (CUF) Hija Hasan Hija .
 
Hija aliyetaka kujua ni kiasi gani serikali imepata hasa na imejifunza nini  kutokana na mamuzi wa wananchi, je ni sheria gani iliyovunjwa na wananchi na je sheria hiyo ilipitishwa au kuridhiwa na baraza la wawakilishi.
 
Aidha Hija alitaka kujua iwapo sheria ipo na inafanya kazi ni kwa nini vyombo va Dola vikaaamua kuwapiga na kuwasumbua wananchi badala ya sheria kuchukua mkondo wake wakati wa zoezi la sensa lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
 
Waziri alisema hasa pale serikali ilipoongeza wiki moja zaidi kwa ajili ya kuendelea na kazi ya kuhesabu watu sio rahisi kupata tathmini ya fedha zilizotumika kughaamia kazi za ziada zilizofanywa na makundi ya watu mbali mbali walihamasisha na kuelimisha watu washiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi baada ya kugomea kuhesabiwa kwa wiki ya kwanza.
 
Alisema sheria iliyovunjwa ni sheria ya takwimu ya Zanzibar Namba 9 ya mwaka 2007 sehemu ya tano kifungu cha 14 (2) na (3) na sheria hii ilipitishwa na Baraza la wawakilishi
 
Mzee alisema serikali haina taarifa kuwa wananchi waliosusia sensa walipigwa  na kusumbuliwa na vyombo vya dola na hakuna mwananchi aliyewasilisha madai ya aina hii katika chombo chochote cha kisheria hapa Zanzibar kinyume chake ni baadhi ya wananchi waliosusia zoezi hilo ndio waliofanya fujo.

“Serikali haina taarifa ya kuwa kuna watu waliyanyaswa kuhusu suala la sensa lakini tunajua kuwa maafisa wa sensa ndio walionyanyaswa, kupingwa na kuharibiwa mali ya serikali ilipokuwa ikifanya hiyo kazi” alisema Waziri.
 
Waliwapiga na kuwatukana makasaa wa sensa kuwanyananya maafisa vifaa vyao vyakufnayia kazi ni wananchi ambao hawakuwa wakitaka kuhojiwa kuhusiana na zoezi hilo la sensa ambapo mbali ya kuhatarisha usalama wa maafisa hao lakini pia wamehatarisha usalama wa wananchi wenzao katika maeneo ya makaazi yao.

Alisema muda wote huo serikali ilichukua busara na hekma kubwa na ilijiepusha na vitendo va kutumia nguvu na iliunda timu ya viongozi wa dini na watu mashuhui kwa leno la kuwaelimisha zaidi wananchi badala ya kuwachukulia hatua.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Chonga Abdallah Juma Abdallah (CUF) alisema sensa imeshindwa kufanikiwa kutokana na tabia ya masheha kukataa kuwatambua wananchi katika maeneo yao wakati wa uchaguzi na ndio wananchi wamejenga uadui kati yao na masheha.

“Mheshimiwa Spika Masheha wamekuwa na tabia ya kukataa kuwatambua wananchi wa maeneo yao katika shehia zao hata kama wanawajua lakini ikifika wakati wa uchaguzi wanasema hawawatambui jee serikali haioni kwamba kittendo cha Masheha ndio kilichochangia wananchi kukataa kutoa ushirikiano kwa Masheha wakilipiza kutotambuliwa kwako na Masheha?” alihoji Abdallah.

Waziri akijibu hilo alisema inawezekana ikawa suala hilo ni kweli lakini akasisitiza ushirikiano mzuri kwa kati ya wananchi na masheha ni serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na masheha ambao wamekuwa hawataki kutoa ushirikiano kwa wananchi ili wananchi waweze kuelewana na masheha kwani bila ya mshirikiano hakuna kazi ya maendeleo itakayofanikiwa.

No comments: