ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 3, 2013

UTUNDU WAKO FARAGHA NDIYO MPANGO MZIMA


AWALI ya yote niwatakie wasomaji wangu wote Heri ya Mwaka Mpya wa 2013. Kwa sisi tuliojaliwa kuuona tukiwa wazima, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa wema wake huo lakini tuzidi kumuomba atuepushie na na yale ya shari na atujalie yale ya heri.
Ndugu zangu, baada ya kusema hayo, nirudi kwenye mada ambayo nimepanga kufungulia mwaka. Mara nyingi nimekuwa nikipata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanawake wakilalama kusalitiwa na wapenzi wao.
Usaliti umekuwa ni kama wimbo wa taifa sasa, hakuna anayeweza kuwa kwenye uhusiano na mtu kisha akawa na uhakika wa asilimia mia kuwa hasalitiwa. Mawazo ya kusalitiwa yamekuwa kwenye vichwa vya wengi.
Ila sasa cha kujiuliza ni kwamba, kwa nini tunasalitiwa? Je, tunakosea wapi mpaka wapenzi wetu wanafikia hatua ya kuamua kusaliti? Kuna sababu nyingi zinazosababisha usaliti lakini leo nataka kuzungumzia ishu muhimu sana kwa wanawake.
Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo ukizifuata kwa ufasaha, huwezi kuumia. Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye amekuzimikia.
Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.
Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii wameachika na bado wanarandaranda mtaani.
Kwa kifupi unapoingia kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi amebahatika kuwa na wewe.
Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi ambayo hakika nikianza kuyajadili hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo nigusie utundu katika uwanja wetu ulee wa kujidai.
Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe kwa kiwango kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo kwa kubaniana kwani ikiwa hivyo lazima mke atakosa furaha aliyoitarajia.
Ila sasa leo nataka niwape darasa huru wanawake. Kuna wale ambao wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda sana na kuwapatia kila wanachohitaji lakini baadhi yao wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata kwingine.
Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi walio ndani ya ndoa siku hizi wanasalitiwa sana. Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji sana lakini wanapokuwa kwenye uwanja wa kujidai unaweza kudhani siyo wao. Hawajui kitu, wamekaa kama magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu, zitadumu kipi?
Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni kama mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike kutoka nje. Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa tayari ulishapendwa na kuwekwa ndani, ipo siku utajikuta ni mke kwa jina tu.
Naomba niseme tu kwamba, huenda unajiamini kuwa ni mzuri na umbo la kuvutia kiasi kwamba, ni rahisi kupata mwanaume wa kukuoa lakini tambua bado utakuwa na kazi kwenye kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi mazingira ya mumeo kutafuta nyumba ndogo.
Hakikisha unaonesha uanamke wako ili hata kama huyo mumeo atatoka nje, iwe ni kwa tamaa zake tu lakini mambo ya msingi uwe unampatia.

www.globalpublishers.info

Ni hayo tu kwa leo, niwatakie Heri ya Mwaka Mpya wa 2013.

1 comment:

Anonymous said...

Lets talk about waume wasioridhisha wake zao,je una mada hiyo? Wanawake nao wameamka,wanatafuta pembeni kiridhishwa,wake up ,tis new era& generation. Siku hizi ni choicw wanawake wako happy kuwa single kuliko kuwa na mme jina si vitendo.Probably u r out of touch.