ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 13, 2013

Wahoji mke wa rais kuanzisha asasi yake

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba 

BAADHI ya wananchi wamehoji wake wa marais wanaoingia madarakani kila mmoja kuanzisha  asasi yake, badala yake wametaka Katiba Mpya iwapige marufuku au iwepo moja ya kitaifa.  
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alisema hiyo ni miongoni hoja  nyingi ambazo zimekusanywa na jukwaa hilo kutoka kwa wananchi mbalimbali nchini.
Kibamba alisema katika hoja hiyo wananchi hao wameshauri kuwa, asasi hiyo iwe ni maalumu kwa ajili ya kusimamiwa na mke wa rais atakayekuwa madarakani kwa wakati husika.
Pia, alisema ilipendekezwa kwamba usawa wa jinsia ufikie uwiano kamili wa 50 kwa 50 kwa kuzingatia itifaki ya mikataba ya Maputo na Umoja wa Afrika, katiba iweke misingi ya kuwezesha kutambua michango ya wanawake kuendeleza uchumi hususan rasilimali watu.
“Hiyo wamependekeza iwekwe ili kuzuia sera zinazoelekeza kumwongezea mwanamke mzingo  mkubwa zaidi, sheria na bajeti kuwekeza katika huduma zitakazompunguzia mwanamke mzigo,” alisema 
Mwananchi

No comments: