Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Francois Bozize, amemtoa kazini waziri mkuu kufuatana na makubaliano ya kusitisha mapigano aliyofikia na wapiganaji.
Nafasi ya Faustin Archange Touadera itachukuliwa na mfuasi wa upinzani.
Ijumaa serikali na makundi ya wapiganaji walikubaliana kuunda serikali ya mseto baada ya mazungumzo ya siku kadha mjini Libreville, mji mkuu wa Gabon.
Kufuatana na makubaliano hayo Rais Francois Bozize atabaki madarakani hadi mwaka wa 2016.
Piya kuna mpango wa kufanya uchaguzi wa wabunge katika mwaka mmoja.
Wapiganaji walianza mapambano mwezi Disemba na walikaribia kuuteka mji mkuu, Bangui.
No comments:
Post a Comment