Mabingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), klabu ya Yanga watapima makali waliyoyapata Uturuki kwa kucheza mechi mbili za kirafiki kuanzia Jumapili dhidi ya timu kutoka Afrika Kusini ‘Sauzi’ na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Yanga ambao walikuwa wameweka kambi ya wiki mbili mjini Antalya, Uturuki kujiandaa kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, walitarajia kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo alfajiri.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrence Mwalusako alisema kuwa timu yao itacheza mechi hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.
Hata hivyo, Mwalusako alikataa kuzitaja timu hizo kwa madai kwamba bado wako katika mazungumzo na kwamba mambo yatakapokamilika, wataweka kila kitu hadharani.
“Kikosi cha wachezaji 27 wa timu yetu (Yanga) kitawasili nchini kesho saa 10:00 alfajiri. Tutakuwa na mechi mbili za kirafiki kabla ya kuuanza mzunguko wa pili,matarajio yetu ni kupata wapinzani kutoka Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo,” alisema Mwalusako aliyesisitiza kuwa tayari wameshaanza mazungumzo kuhusiana na mechi hizo.
Yanga waliondoka nchini Desemba 29 kuelekea Uturuki ambako waliweka kambi yao ya wiki mbili kunoa makali yao katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ambayo wanaongoza katika msimamo wakiwa na pointi 29.
Wakiwa Uturuki, Yanga walicheza mechi tatu za kirafiki. Walipata sare ya 1-1 katika mechi yao ya kwanza dhidi ya timu ya Arminia Bielefeld iliyowahi kucheza Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).
Katika mechi ya pili iliyochezwa kwenye uwanja wa Selen Football, Yanga walikubali kipigo cha 2-1 kutoka kwa timu ya Denizlispor inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Uturuki.
Katika mechi ya mwisho dhidi ya Emmen inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Uturuki, Yanga ililala tena kwa magoli 2-0 kwenye uwanja wa Adora Football, Berek mjini Antalya.
Yanga inakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mabingwa wa mwaka huu wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC wanaokalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wakiwa na pointi 25, moja zaidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Simba ambao wanaendelea na kambi yao nchini Oman kujiandaa kwa mzunguko huo.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment