Mshambuliaji wa Ghana, Asamoah Gyan (mwenye jezi nyeupe) akiwania mpira na Paul Koulibaly wa Burkina Faso wakati wa mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa Afrika kati ya Ghana na Burkina Fasoleo katika Uwanja wa Mbombela, Nelspruit nchini Afrika Kusini. Burkina Faso wamefanikiwa kutinga fainali kwa ushindi wa penati 3-2.
Elderson Echiejile wa Nigeria akishangilia bao lake pamoja na wachezaji wenzake wakati wa mechi ya Nusu Fainali kati ya Nigeria na Mali iliyopigwa katika Uwanja wa Moses Mabhida jijini Durban, Afrika Kusini. Nigeria wameshinda bao 4-1 na kutinga fainali ya michuano hiyo.
Christian Atsu wa Ghana (7) akijaribu kumtoka beki wa Burkina Faso, Bakary Kone wakati wa mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika leo katika Uwanja wa Mbombela, Nelspruit nchini Afrika Kusini. Burkina Faso wameshinda kwa penati 3-2 na kutinga fainali.
Mahamadou Samassa wa Mali (katikati) akiwania mpira na wachezaji wa Nigeria, Reuben Gabriel (kushoto) na Efe Ambrose (kulia) wakati wa mechi ya Nusu Fainali kati ya Nigeria na Mali iliyochezwa katika Uwanja wa Moses Mabhida jijini Durban, Afrika Kusini. Nigeria wameshinda kwa bao 4-1 na kutinga fainali.
(PICHA ZOTE NA MTN FOOTBALL)
No comments:
Post a Comment