Kikundi cha Utamaduni cha Mkoa wa Singida kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya mlezi wa mkoa huo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Mara baada kuwasili Mkoani humo kwa ajili ya kuongoza matembezi ya mshakamano kutimia miaka 36 tokea kuzaliwa kwa CCM Mwaka 1977.
Mlezi wa Mkoa wa Singida kichama ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akipanda mti wa kumbu kumbu akiwa sambamba na mmiliki wa mradi huo Nd. Katala Kitila mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Katala Beach Hoteli Mjini Singida.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiashiria kuweka jiwela la Msingi la ujenzi wa Mradi mkubwa wa Katala Beach Hoteli uliyopo pembezoni mwa Bwawa la Singidan Mjini Singida ikiwa shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM
Pembeni ya Balozi ni Mmiliki wa Mradi huo ambao hadi sasa umeshagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 1.3 ambae pia ni Kada wa Chama cha Mapinduzi Nd. Katala Kitila.
Mlezi wa Mkoa wa Singida Kichama Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi ameweka jiwe la Msingi la Mradi Mkubwa wa Katala Beach Hoteli unayojengwa pembezoni mwa Ziwa la Singidan Mkoani Singida.
Mradi huo ambao hadi sasa umeshagharimu zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 1.3 umeanzishwa na Mfanyabiashara Mmoja ambae pia ni Mwanachama wa CCM Mkoani Singida Ndugu Katala Kitila.
Zaidi ya Vijana 70 wanatarajiwa kupata ajira mara baada ya kukamilika kwa mradi huo ambao unatarajiwa kuwa na vyumba 30 kwa awamu ya mwanzo ya ujenzi huo.
Akitoa taarifa fupi ya ujenzi huo Mmiliki wa Mradi huo Bwana Katala Kitila alisema lengo la kuanzishwa kwa mradi huo ni kuifanya Singida kuwa sehemu ya kuishi hasa Vijana badala ya ile tabia ya kukimbilia Mijini.
Bwana Katala alisema mradi huo mbali ya huduma za hoteli lakini pia unatarajiwa kutoa huduma za michezo ya watoto, burudani, huduma za kibengi ili kusaidia kuchangia pato la Mkoa .
Hata hivyo Bwana Katala alisema zipo changamoto kadhaa zinazokabili harakati za kiuchumi ndani ya Mkoa wa Singida akizitaja kuwa ni pamoja na upatikanaji wa mikopo na ufinyu wa bara bara mambo ambayo iwapo yatapatiwa ufumbuzi Mkoa huo una uwezo wa kubadilika haraka.
Akizungumza na Viongozi na wanachama wa Mkoa wa Singida mara baada ya kuwasili mkoani huo kwa ajili ya matembezi ya mshikamano Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif aliwataka viongozi na wanachama hao kujiepusha ili kukijengea nguvu zaidi chama chao.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mlezi wa Mkoa wa huo wa Singida alisema kazi iliyo hivi sasa ndani ya CCM ni kwa wanachama na Viongozi wake kujipanga vyema kwa lengo la kujihakikishia ushindi kwenye uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015.
Alieleza kwamba amani na utulivu ndani ya ardhi ya Tanzania haitapatikana kamwe iwapo chama cha Mapinduzi hakitashika dola la kuongoza Nchi kauli ambayo hata Baba wa Taifa Marehemu Mwalimu Julius Nyerere alikuwa aliyasisitiza.
Mapema Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida Bibi Naombi Mpambala akitoa Taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM Mkoa humo alisema yapo maendeleo makubwa yaliyopatikana ndani ya Jamii katika kipindi cha miaka 36 tokea kuzaliwa kwa CCM.
Bibi Naomi alisema Mkoa wa Singida ulikuwa na skuli za msingi 274 mwaka 1977 wakati hivi sasa tayari zipo skuli 511 na kwa upande wa sekondari zilikuwa zilikuwepo mbili mwaka 77 wakati hivi sasa zilizop[o ni 173.
Katibu huyo wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida alifahamisha kwamba uongozi wa chama hicho mkoani humo umejipanga kujiimarisha zaidi kiuchumi katika mipango yake ya baadae.
Hata hivyo alieleza kwamba zipo changamoto zilizojitokeza ndani ya chama kwa kipindi hichi ambazo ni kwa baadhi ya wapinzani kujipenyeza ndani ya chama na kutaka uongozi wa nia ya kudhoofisha nguvu za chama hicho.
No comments:
Post a Comment