Saturday, February 2, 2013

CCM yaonyesha hofu ya kufikia lengo la Ilani 2025


Dk Msengi alisema, hofu hiyo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM imeonyesha kwa halmashauri hiyo kutokana na kuwapo kwa uchakavu wa baadhi ya miradi kwa kuwa ni ya miaka mingi tangu

ILANI ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005-2012 imeonyesha wasiwasi wa kutofikiwa kwa lengo na mtazamo, ifikapo mwaka 2025 ambapo watu wote wawe wanapata maji safi na salama kwa umbali usiozidi mita mia nne.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Dk Ibrahim Msengi alipokuwa akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Ilani hiyo kwa viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaroli kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya na kuhudhuriwa pia na waandishi wa habari mkoani hapo.Dk Msengi alisema, hofu hiyo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM imeonyesha kwa halmashauri hiyo kutokana na kuwapo kwa uchakavu wa baadhi ya miradi kwa kuwa ni ya miaka mingi tangu ilipojengwa ukilinganisha na ongezeko la watu na mahitaji ya maji, hivyo miradi hiyo kushindwa kukidhi mahitaji hayo.

Mkuu huyo wa wilaya alitaja baadhi ya sababu nyingine zinazoonyesha kutofikiwa kwa lengo hilo kuwa ni uharibifu mkubwa wa mazingira ambao Dk Msengi alibainisha kuchangiwa kwa kukauka au kupungua kwa baadhi ya vyanzo vya maji na baadhi ya wananchi kudaiwa kukataa kuchangia huduma za maji kwa dhana kwamba maji ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Alisema pamoja na jitihada za kuwahamasisha wananchi hao kuanzisha vyombo huru vya kusimamia na kuendesha miradi ya maji iliyopo,wananchi wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya miradi iliyopo kuwa chakavu.

Dk Msengi alitaja baadhi ya mikakati ya kukabili hofu hiyo kuwa ni pamoja na halmashauri kuhamasisha wananchi .

Mwananchi.

No comments: