Tuesday, February 5, 2013

CHUO KIKUU CHA DODOMA KUANZA KUFUNDISHA KICHINA

Chuo kikuu cha Dodoma kimethibitisha kwamba Kozi ya lugha ya kichina itaanza kutolewa kwenye chuo hicho ambapo makamu mkuu wa chuo Profesa Idris Kikula amesema uamuzi huo umetokana na kukua kwa ushirikiano wa wafanyabiashara wa China na wafanyabiashara wa Tanzania.

thecitizen.co.tz wameripoti kwamba Profesa kasema chuo chake kilikua na malengo ya kuandaa walimu ambao watakua wakifundisha lugha ya kichina kwenye shule za sekondari Tanzania pamoja na taasisi nyingine za elimu.

Info za uhakika ni kwamba mwaka 2006 wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wasiozidi laki mbili walikwenda China kujifunza kichina, na wakati huohuo watu wapatao milioni 20 sehemu mbalimbali duniani wameshajifunza lugha ya kichina

No comments: