Saturday, February 9, 2013

DIAMOND KATIKA PENZI ZITO NA VJ PENNY PICHA ZA MPENZI WAKE HUYO AMBAZO ALIZIANDIKIA UJUMBE WA MALAVIDAVE UKIJIELEZA LABDA AMESHASHIKA VIMAREKANI VYA MIMBA


Ikiwa ni jana tu, Raisi Wa Wasafi, Diamond Platnumz alitupia picha katika moja ya mitandao ya jamii anayotumia, huu ukiwa ni Instagram ya mtangazaji wa kipindi cha Xtreme kituo cha TV cha DTV, Pennyl Mungirwa a.k.a Penny ikiwa na maandishi chini yake yanayoonesha wawili hawa sasa wako katika mahusiano ya kimapenzi.
Diamond anaetamba sana kwa sasa na wimbo wake wa Kesho uliofanyika MJ Records chini ya Marco Chali na video yake kufanywa Nairobi, Kenya ali-post picha hiyo ikiwa na maandishi au Hashtags "#MaBabyMama De'MumOfMyBlood #MamaYounDiamond #YounPlatnumz #YounPrezident" yaliyozidi kuweka wazi kuwa wawili hawa wako pamoja kimapenzi.
Bofya kuona picha za tunda hilo jipya la Platnumz
Katika hali iliyozua maswali zaidi, moja ya Hastags hizo, zilionesha VJ Penny ana ujauzito wa Diamond Platnumz... Je ni kweli?? Maandishi hayo yalisomeka, "#MaBabyMama De'MumOfMyBlood"

Wawili hawa wamekuwa wakishukiwa kuwa kwenye mapenzi kutokana na picha tofauti ziliwaweka katika mapozi yaliyoonesha hivyo lakini muda mwingi hawakutaka kuyaongelea haya na mara mara walionekana kukanusha kabisa habari hizo.

No comments: