ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 26, 2013

HABARI KAMILI JUU YA MWANAMUZIKI WA BONGOFLAVOR KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO BURUNDI

Timbulo
Leo kumekua na story zilizoenea mitaani kuhusu Mwanamuziki Timbulo kukamatwa na madawa ya kulevya Nchini Burundi. Baadhi ya watu wanas3ma wameona picha kupitia mtandao wa facebook ambazo zimemuonyesha timbulo akiwa chini ya ulinzi wa police na kidhibiti chake cha madawa haya ambayo yamefungwa kwa mfano wa pipi?

Ilinibidi nimtafute timbulo kupitia mtandao wa whatsup ambapo nilimuona akiwa active kama dkk kumi zilizopita mara baada ya kupata habari hizo

Timbulo amesema ni kweli alihisiwa kuwa amebeba madawa ya kulevya kitu kilichowafanya wanausalama kuomba kumkagua na kweli kumkuta na Pipi ambazo mara nyingi zimekua ni mfumo wa kubebea madawa ya kulevya katika begi lake, lakini katika maelezo ya timbulo anasema hazikuwa dawa za kulevya kweli bali ni mfano wa dawa ambazo alifanyia shooting katika movie yake ya hivi karibuni na kusahau kuzitoa. Hata hivo kutokana na maelezo yake anasema alihisiwa zaidi kubeba mzigo huo kutokana na mtu aliekuja kumpokea kusadikika kuwa katika biashara hiyo.

Timbulo alikua nchini burundi kwa shughuli zake za kimuziki akiwa ametokea Bukoba alikokua na shows huko lakini pia ikiwa ni mwendelezo wa safari ya kumfikisa Younde Cammeron ambako pia alikua anaenda kwa shughuli zake za kimuziki. Safari zote hizo ziliishia hapo baada ya tukuo hilo na hivi mpaka naingia mtamboni timbulo aliniambia yupo jijini mwanza kwa safari ya kurudi Dar Es Salaam.

No comments: