Sunday, February 3, 2013

JENGO LA PPF TOWER LASHIKA MOTO ASUBUHI HII


Picha ya jengo la PPF ikionesha moshi mkubwa unaofuka kutoka kenye jengo hilo (Shukurani ya picha: A, rafiki wa M.C.
Jamani hapa tetemeko limetukumba katika Jengo letu lakini tupo salama ndivyo anavyowasimulia jamaa na ndugu kwa simu huyu dada.(picha hizi ni siku wafanyakazi wa jengo hilo walipotimua mbio kwa tetemeko)
wafanyakazi wanaotumia jengo hilo wakiwa nje
Habari kutoka jijini Dar es Salaam ambazo zimetua katika mtandao huu hivi punde na kurushwa moja kwa moja na kituo cha radio Nuru Fm 93.5 Mhz kupitia mwandishi wetu Dotto Mwaibale zinadai kuwa jengo la PPF TOWER lililopo katikati ya jiji la Dar es Salaam kwa sasa linaendelea kuteketea kwa moto .
Tukio hilo limetokea majira ya saa 1.30 asubuhi ya leo baada ya walinzi wa jengo hilo kushuhudia moshi mzito ukitoka kutoka ndani ya jengo hilo katika ghorofa ya mwisho na hivyo kulazimika kutoa taarifa vikosi vya zimamoto .
Hata hivyo inadaiwa kuwa kikosi cha jeshi la zimamoto na uokoaji wamefika mapema zaidi eneo la tukio na askari wake kufanikiwa kupanda hadi juu ya ghorofa hiyo ambako moto huo ulianzia kuwaka ili kujaribu kuzima japo shida kubwa ni mpira wa maji kufika katika eneo hilo.
Kwani katika eneo hilo ambako pia kuna mitambo mbali mbali ya mawasiliano imefungwa ila mbali ya kutumia winchi kupandisha mpira huo wa maji bado imekuwa ngumu kufika juu ya ghorofa hilo.
Hivyo moja kati ya changamoto ambazo zimetajwa kwa wajenzi wa majengo ya ghorofa jijini hapo ni kujenga majengo hayo huku wakichukua tahadhari na matukio ya moto pia .
Mwaibale amesema kuwa hadi sasa eneo la tukio askari wametanda kila kona ili kupambana na vibaka ambao wamekuwa na kawaida ya kupora mali katika maeneo ya matukio kama hayo na kuwa hakuna madhara yaliyojitokeza kwa binadamu japo thamani ya mali zinazoendelea kuteketea bado kujulikana na jitihada za kuzima moto zinaendelea

No comments: