Na Mwandishi Wetu
WAKATI Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likifanya kazi ambayo ingefanywa na Simba ya kuwapokea wachezaji na viongozi wa timu ya Recreativo do Libolo ya Angola, timu hiyo imeonekana kuwadanganya Simba.
Timu hiyo ambayo ilianza kuwasili hapa nchini kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita, imekuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam kwa maficho sana.

Hata hivyo, kwenye mazoezi yao wamekuwa wakifanya mambo ambayo ni sawa na kuwahadaa Simba ambao watapambana nao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumapili ijayo.
Kocha wa timu hiyo, Zeca Amaral, ambaye amekuwa akigoma kuzungumza na waandishi wa habari mara kwa mara, amekuwa akiwafanyisha wachezaji wake mazoezi rahisi sana lakini wakati mwingine amekuwa akiwatumia washambuliaji kama mabeki na mabeki kama viungo ili kuwadanganya Simba ikiwa wametuma watu wao kuwachunguza.
Kwa mujibu wa majina ya wachezaji hao, Manuel António Machado ni beki, lakini mara nyingi kocha huyo amekuwa akimtumia mazoezini kama mshambuliaji, nafasi ambayo ameonekana haimudu vyema. Reginaldo da Silva Santos ambaye pia ni mshambuliaji, amekuwa akitumiwa kama beki mara kwa mara.
Hata hivyo, ili kuonyesha kuwa wanawahadaa Simba, wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakifurahia kila wanapokuwa kwenye nafasi hizo ambazo siyo zao, lakini siri imefichuka kwa kuwa wamekuwa wakiitana majina wakati wa kuomba mipira.
Lakini hata mazoezi ambayo wamekuwa wakifanya ni ya muda mchache sana na wakati mwingine yamekuwa yakifanana.
“Hawa jamaa wanawadang’anya Simba, timu kubwa kama hii haiwezi kufanya mazoezi ya namna hii, huu ni uongo,” alisema shabiki mmoja nje ya uzio wa uwanja huo.
GPL
No comments:
Post a Comment