Monday, February 4, 2013

Mama Anne Kilango na Ajira za Emirates-Watanzani ni 9 tu, Wakenya watupiga Gap

Bungeni patamu!

Muda mfupi uliopita mama Anne Kilango amemaliza kuchangia hoja ya jinsi gani vijana wasaidiwe kupata ajira. Kama kawaida yake ameirarua serikali.Amesema kuna siku amesafiri na ndege ya shirika la Emirates, mle ndani alikutana na mfanyakazi mtanzania anaitwa Felister.

Mama Anne Kilango alimdadisi yule dada hadi akamwambia kati ya wafanyakazi 15,000 wa shirika lile wapo watanzania 9, wakenya 800, sababu ni kuwa wakenya nafasi zikitoka serikali yao inaintervene kuwatafutia vijana wake. Mama Kilango anasema huo ni uzembe wa serikali yetu.

Mara palepale mbunge MACHALI akaomba kutoa taarifa na bahati mbaya naibu spika akamruhusu, Machali akampa taarifa mama Kilango kuwa "Kenya wamefikia pale kwa sababu walifanikiwa kukiondoa chama tawala madarakani".

Majibu ya mama Kilango yalikuwa ya aibu maana kwa kujivuta na ile sauti yake ya mkwara akasema."Taarifa hiyo naifuta na wala sitaki kuisikia"

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake