POLISI mkoani Mwanza wanamshikilia Imamu wa Msikiti wa Ijumaa, huku likitangaza kuwasaka masheikh wawili wengine pamoja na Askofu (majina yote yanahifadhiwa) kwa kuhusika na uchochezi wa kidini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alisema Imamu huyo wa msikiti alitiwa mbaroni kwa madai ya kubainika kwamba wanahusika na usambazaji wa CD za uchochezi ambazo zimekuwa zikihamasisha vurugu pamoja na mauaji ya kidini ikiwa ni pamoja na suala la kuchinja.
Kwa upande wake Askofu Mpemba wa Kanisa la Tanzania Field Evangelist yeye anasakwa kutokana na kutoa mkanda wa video (DVD) yenye jina la ‘Inuka Chinja Ule’ wakati mashehe wawili wanasakwa kwa kuhusika na uandaaji wa mikanda ya video mitatu (DVD) zenye majina ya ‘Unafiki katika Sensa, Kadhia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na Uadui wa Makafiri’.
Wakati huohuo, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Morogoro, limesema huenda likajitenga na Bakwata Taifa kufuatia hatua ya Sheikh Mkuu, Mufti Issa Shaaban bin Simba kumvua madaraka Sheikh wa Mkoa wa Morogoro, Yahya Semwali bila kufuata utaratibu.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment