Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limekamata na kumhoji Mwinjilisti mmoja wa Kanisa la Moravian Tanzania kwa tuhuma za kuhubiri kwa kutumia maneno ya uchochezi dhidi ya dini nyingine, hali ambayo inahatarisha amani ya nchi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Nicholaus Kamwangila (35), mkazi wa Mtoni Mtongani, Dar es Salaam.
Alisema Muinjilisti huyo alikamatwa juzi jioni wakati akiendelea na mahubiri yake katika Kanisa la Moravian Ushirika wa Iyunga jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa Kamanda Diwani, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na CD pamoja na vipeperushi ambavyo vinaendelea kuchunguzwa na Polisi.
Kamanda Diwani alisema maneno ya uchochezi aliyokuwa akiyatumia hayakuwafurahisha baadhi ya waumini, ndipo wakatoa taarifa polisi.
Alisema kuwa baada ya polisi kupata taarifa, walikwenda kwenye kanisa hilo na kumkuta mwinjilisti huyo akiendelea na maubiri yake nje ya kanisa ndipo walipoamua kumkamata.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment