Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu (wa pili), akikagua gwaride la askari wapya 822 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wakati wa kufunga mafunzo yao ya miezi sita kwenye uwanja wa Mlale JKT jana. Kushoto ni Kamanda wa gwaride hilo Meja Aman Ramadhan.
Na Liberatus Mwangombe/ RaiaTahadhari!!!!!Tumia akili zaidi kuliko HISIA kuelewa kilicho andikwa hapa, unaweza kuwa na mawazo tofauti na yangu, ni sawa. This is how democracy works.
NAPINGA WABUNGE KWENDA JKT
Nimesikia kwa muda kuwa wabunge watajiunga na JKT. Nilipata kuona baadhi ya comments kuwa ni wazo zuri, LAKINI, nitaomba kutofautiana na wengi kwa sababu zifuatazo;
Nne: Kama ni uzalendo wa kweli, ilipaswa wajiunge na jeshi wakiwa vijana au kabla hawaja anza kuwatumikia wananchi. Na maanisha kama JKT ilikuwa haipo, wangejiunga hata na Polisi au Jeshi la ulinzi la Tanzania (JWTZ). Kuna viongozi ambao walipitia JKT, lakini hawana uzalendo na ni MAFISADI number one. Tazama nchi zilizo endelea, wanapita Jeshini kwanza na baadaye wanaanza kuwatumikia raia kwa kuwarepresent bungeni n.k. Mfano, John Mcain, senator in USA, au John Kerry ambaye sasa ni Secretary of State America.
Tano: Nimeona wanatoa sababu ya kujiunga na jeshi kuwa ni kujifunza kazi za kila siku za maisha, kiuchumi, kijamii na nidhamu. Guys! Give me a break. Kama umeshakua Mbunge na unategemea kwenda kujifunza nidhamu ukiwa bungeni, tafadhari kaa chini na re-think. Uchumi na mambo ya kijamii, kwa nini usisome vitabu na research kwa wananchiunao waongoza.
Sita: Kama wanataka kujiweka fit, kwa nini wasibadirishe style ya maisha. Kula vizuri, kuacha sigara, kupunguza pombe, kujiunga na gym, na kuelekeza nguvu zaidi kwenye kuwatumikia wananchi.
Mwisho: Naomba mh. Raisi aingilie swala hili na kusitisha ili kuokoa GHARAMA, MUDA na NGUVU za waTanzania.
1 comment:
Kaka Liberatus, nimekupata straight na nakuunga mkono. Wabunge wa TZ wameshakithiri na ukosefu wa upeo wa kufikiri, inasikitisha....Mdau Haji Jingo, California.
Post a Comment